Cardinal06
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 963
- 326
Fidelis Butahe na Sharon Sauwa mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Chama cha Wananchi CUF, kimemtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kutojaribu kukiyumbisha chama katika kipindi hiki ambacho nchi ina matatizo lukuki.
Kauli hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF Taifa, Twaha Taslima imekuja baada Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu mwaka jana, kutengua uamuzi wa kung’atuka CUF na kuomba kurejea kwenye wadhifa wa uenyekiti wa chama. Taslima ambaye amethibitisha kuwa atagombea uenyekiti wa CUF katika uchaguzi huo uliopangwa Agosti 21, amesema wanachama wa chama hicho wanajiuliza maswali mengi baada ya uamuzi huo wa Lipumba. Amesema hakuna kipengele cha katiba ya CUF kinachosema mwenyekiti akijiuzulu anaweza kusitisha mpango huo na kurejea katika wadhifa wake. “Hakuna kipengele cha Katiba ya CUF kinachosema mwenyekiti akijiuzulu anaweza kusitisha mpango huo na kurejea katika wadhifa wake. Ombi la Lipumba halitekelezeki,” amesisitiza.
.
.
Chanzo: Mwananchi