Mkuu Mkandara,
Ni kweli kabisa unayosema hujaenda mbali sana na Prof. Lipumba, ndiyo maana nikasema hawa jamaa inafaa waondoke tu, tatizo wananchi hawapo tayari chama kipo ndani ya damu yao, hawajali njaa zao na shida, wao bendera na shina la chama vinawatosha, hawajali zahanati, shule bora kwa watoto wao wala vipi. Ndiyo nasikitika Watanzania wanajitakia wenyewe kuwa masikini.
Mkuu, Republican wameondoka madarakani baada ya miaka kumi tu ya utawala wa Bush, na sikuwa hawajajenga bara bara, madaraja na vyuo vikuu...la hasha, watu wanataka mabadiliko tu na mitazamo mipya ya kimaendeleo. Imagine hawa ni watu wenye maendeleo makubwa kabisa, how come sisi tunakaa na chama miaka zaidi ya 40 plus na matatizo yote uliyoyasema mkuu, wananchi wapo taabani....bado chama hicho hicho kina guarantee ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao....Mkuu mi hapa naganda nashindwa kushangaa.