maonomakuu
JF-Expert Member
- Jul 24, 2015
- 2,516
- 1,198
Akiongea mchana huu kwa taarifa uliyorushwa na kituo cha Azam TV kuwa hajui sababu hasa ya mgogoro huo.
=====
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, leo ameadhimisha kumbukumbu ya wahanga wa maandamano ya amani ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2000 yaliyofanyika visiwani Pemba, Januari 26 na 27,2001.
Prof. Lipumba amesema maandamano hayo yalisabaabisha vifo vya watu sitini hususan wafuasi wa CUF waliofariki dunia wakati wakishiriki katika maandamano hayo huku watu zaidi ya 2000 walikimbia makazi yao kutoka Zanzibar hadi Mombasa nchini Kenya.
Lipumba ametoa rai kwa viongozi wa CUF kukumbuka na kuenzi mchango wa wahanga hao ambao walijitoa kwa ajili ya kudai haki, demokrasia ya kweli, katiba pamoja na tume huru za uchaguzi kuanzia ya Zanzibar (ZEC) hadi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (NEC).
Hata hivyo, amedai kuwa chama cha CUF kimerudi nyuma kisiasa baada ya kupita uchaguzi Mkuu wa 2015, kutokana na mgogoro uliopo sasa, uliosababisha mpasuko wa viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na kukosa nafasi za uwakilishi 27, Zanzibar ambazo wawakilishi wake walishinda na kupatiwa vyeti vya ushindi.
Amesema licha ya wawakilishi hao kupatiwa vyeti vya ushindi, ZEC iliamuru uchaguzi wa Zanzibar urudiwe na kwamba CUF iligoma kurejea uchaguzi huo, huku Baraza lake Kuu la Uongozi Taifa likishindwa kutoa amri kwa mawakili wa CUF kufungua kesi ya kupinga wawakilishi wake kurudia uchaguzi ili wabaki na uwakilishi wao.
“Sasa tumerudi nyuma kisiasa baada ya uchaguzi 2015 Zanzibar kufutwa, wawakilishi walipata hati ya kushinda uwakilishi, Wangefungua kesi wangeshinda lakini Katibu Mkuu Maalim Seif Sheriff Hamad alishindwa hilo, mawakili hawakupeleka hoja ya kupinga uchaguzi, ukarejewa hatimaye CCM ikabeba viti vyote ikiwemo na ilivyoshinda CUF,” amesema.
Lipumba amewataka viongozi wa CUF kuungana pamoja kukijenga chama huku akimsihi Maalim Seif kurejea ofisini kwake kwa ajili ya kufanya shughuli za chama.
Chanzo: Dewji Blog