Prof. Lipumba atoa tahadhari kuhusu sera ya gesi na Mafuta. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba atoa tahadhari kuhusu sera ya gesi na Mafuta.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Sep 10, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3]MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amewatahadharisha Watanzania kuhusu upatikanaji wa rasilimali za gesi na mafuta.[/h]Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana, kuzindua kampeni yao ya Vision For Change (V4C), Profesa Lipumba alisema nishati hiyo imekuwa ikisababisha mapigano na mapambano.
  Ameitaka Serikali kuhakikisha nishati hiyo badala ya kugeuka laana kwa Watanzania, imnufaishe kila Mtanzania.
  Akizungumzia miradi mbalimbali ya maendeleo, Profesa Lipumba alidai imekuwa ikipoteza fedha za walipakodi na kushauri ikiwezekana fedha hizo wagawiwe wananchi.
  Profesa Lipumba pia alizungumzia mapinduzi ya kijani na kusema kuwa hayawezi kufanikiwa kwa kuwashirikisha wakulima wadogo na wakubwa.
  Badala yake Profesa Lipumba alitaka mkulima mdogo awe mlengwa wa mapinduzi ya kijani na asaidiwe kupata mbegu, mbolea, zana na upatikanaji wa soko na kutoa mfano wa China Thailand na Indonesia ambako mapinduzi ya kijani yalifanyika kupitia mkulima mdogo.
  Alisema mkulima mkubwa akitakiwa kumsaidia mdogo, atamnyangÂ’anya ardhi, kumfanya kibarua na hataweza kuendelea. Kuhusu wafugaji, alisema wakisaidiwa watatoa mchango katika kuanzisha viwanda vitakavyoondoa tatizo la ajira ambavyo hutumia malighafi ya ndani

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kwanini asipublish nyingine zipatikane katik public na nyingine aipelekee serikaali anayoitaka kama yeye na CUF hawana mpanago wa kuyafanya hayo?
  Blah blah majukwani hatuwezi angalia na kufuata kwa makini.
   
Loading...