Prof. Lipumba amemteua Mbarouk Seif Salim kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

CUF Habari

Verified Member
Dec 12, 2019
239
250
FB_IMG_1606919222276.jpgTAARIFA KWA UMMA
Mwenyekiti wa CUF- Chama Cha Wananchi Prof. Ibrahim H. Lipumba , kwa kutumia Mamlaka yake ya Kikatiba, amemteua Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar kuanzia leo Desemba 2, 2020 kupitia barua yenye kumbukumbu Na. CUF/AK/DSM/MKT/07/2020.

Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Ali Makame Issa ambaye Uteuzi wake ulitenguliwa Novemba 8, 2020 kutokana na kwenda kinyume na Msimamo wa Chama.

Kabla ya Uteuzi huu Mheshimiwa Mbarouk Seif Salim alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.

CUF- Chama Cha Wananchi kinampongeza Mhe. Mbarouk Seif Salim kwa Uteuzi huu na kinamtakia Utekelezaji mwema wa Majukumu yake kama Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Eng. MOHAMED NGULANGWA
Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Desemba 2, 2020
 
Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
122
250
IMG-20201202-WA0081.jpg

TAARIFA KWA UMMA

chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,325
2,000
Ninyi madalali na vipenyo mmeliua lichama lenu, limebaki kama kikundi cha kusaidiana kwenye raha tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom