Prof. Kitila Mkumbo, muogope Mungu!

Prof. Kitila Mkumbo, muogope Mungu!

Tatizo wafuasi wa UKAWA hawapendi kusikia habari mbaya kuhusu UKAWA na LOWASSA. Hata penye ukweli hukataa. Badilikeni siasa siyo hivyo. Wenzenu CCM mapungufu ya upinzani huyafanyia kazi. Hata hawataki kusikia habari za utafiti.punguzeni chuki kwanza na mehemko na mjifunze ustaarabu siyo kila kitu lazima kutukana.
 
Maprofesa wa Tanzania bwana! Eti watu wa vijijini wanachambua sera kuliko wa mijini!! Makubwa!
 
Unaweweseka bure! makala ya proff Kitila ameweza kujikita na kufikiria kama watanzania walio wengi ambao si mashabiki au wafuasi wa UKAWA wanavyoyaona mambo mbali mbali..... Salary slip mahaba yako kwa LOWASA yameifanya akili yako itake kulazimisha mambo au la ndio mwisho wa upeo wako....mnatakiwa mrudi darasani mjitathimini kwa dhati kuwa ni kitu mlikosea hadi mkapata kipigo mlichokipata!! Sasa ni wakati wa kufanya kazi!!!
 
Huyu prof anaongozwa na mahaba kwa chama flani hivi sikitaji ; thats why anaandika porojo
 
Naona kama mmepagawa au dili zenu haziendi sawa? Kukaa meza moja na mafisadi ni laana kubwa sana mmeona yaliyowakuta sasa mtakoma na hilo fisadi lenu.

kama unavosema chadema kukaa na fisadi letu yaani moja laana kubwa sasa nyinyi nyote ni mafisadi watupu waliouza migodi wanaouza nyara wanaouza cocain walochota epa escrow meremeta tan gold radar helicopters ndege ya rais bomba la ges. vp apo laana yenu ni kiasi gani
 
ndio maprofesa wa aina hio wapo wengi kwa kazi hiyo kwani sasa utasikia kila mmoja ni profesa ni dr. lkn nchi ina nini zaidi ya madeni juu ya rasilmali zote ilizokuwa nazo bora sisi tunaojituma kuvuta matoroli na maguta tunazalisha kuliko hao wenye majina ya taaluma kumbe hawana lolote wanapewa hizo sifa kwa kazi maalum
 
Katika Makala aliyoiandika katika ukurasa wa 6 wa gazeti la Raia Mwema la leo tarehe 4/11/2015 yenye kichwa cha habari, "Jinsi wapiga kura wa vijijini walivyomwibia Lowassa" , Prof.Mkumbo anajaribu kuelezea sababu za Lowassa na CHADEMA kwa ujumla kushindwa katika kinyang'anyiro cha uraisi.

Hapa nitatoa summary tu ya kile alichoandika.

Prof.ameeleza mambo kadhaa yaliyochangia Lowassa kushindwa katika uchaguzi huu ikiwa ni pamoja na kupuuza tafiti alizoziita za kisayansi za Twaweza na IPSOS.

Prof.anasema kutokana na tafiti hizi kuonyesha kwamba Dr.Magufuli alikuwa anaungwa mkono zaidi na makundi manne makuu: vijijini,wanawake,wenye umri mkubwa na ambao hawajasoma sana.

Prof.katika makala yake anaendelea kusema kwamba,baada ya matokea hayo,alitarajia Ukawa na mgombea wao wangewekeza nguvu zaidi vijijini kuyalenga hayo makundu lakini wao waliendelea kuwekeza zaidi mijini.

Kwa maoni yake Prof.anasema, Lowassa amekosa kura za wapiga kura wa vijijini kwasababu kuu mbili.Mosi,ni wafuasi wa Lowassa kukataa kuyaona na kurekebisha makosa ya msingi katika kampeni zao.

Kwa mfano,Lowassa akifungua kampeni za kuomba kuteuliwa na CCM mjini Arusha alimwagia sifa lukuki Raisi Kikwete katika mkutano huo ambao ulionekana mpaka vijijini kupitia Television na baadae alipojiuinga Ukawa akageuka na kuponda utawala wa CCM na Kikwete kwamba ameua uchumi wa Taifa.

Pili,ni viongozi wa CHADEMA kubeba agenda ya ufisadi na kuja kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea wao.

Prof.anasema,wapiga kura wa mjini waliokuwa wanataka mabadiliko hawakuona mkanganyiko wowote katika kauli za Lowassa.Lakini wapiga kura wa vijijini wana utaratibu wa kutunza kumbukumbu na kuzitumia wakati muafaka.

Prof. pia anasema wapiga kura wa vijijini, tofauti na wa mjini, waliona swala la viongozi wa CHADEMA kumsimamisha Lowassa ni ukigeugeu wa karne na kuuzingatia uamuzi wao wa Oktoba 25.

Prof.katika Makala yake hiyo,anaendelea kuwasifu watu wa vijijini kuwa eti ni wagumu kubadilika kirahisi kwa kudanganywanywa na ndio sababu hawakumpigia kura Lowassa.

Prof.ananishangaza zaidi pale anapoandika katika Makala yake hiyo kuwa,"wakati watu wa mijini waliamini mabadiliko na kuitoa CCM madarakani,wananchi wa vijijini walionekana kuzingatia zaidi sera na umakini wa wagombea katika kupiga kura".

Maswali yangu kwa Prof. na kwanini nasema amuogope mungu ni haya.

1.Prof. ni kweli una amini wananchi wa vijijini wanazingatia zaidi sera katika kupiga kura na kuchagua viongozi kuliko wananchi wa mijini?

2.Prof.kama kweli watu wa vijijini wanazingatia sera,je, kati ya CCM na vyama vya upinzani(Ukawa) ni chama kipi kilikuwa na sera rafiki zaidi kwa watu wa vijijini?

Je,ni yule aliehubiri elimu bure mpaka chuo kikuu au yule aliehubiri elimu bure mpaka kidato cha nne?

Prof.sera ya CHADEMA ya mwaka 2010 ya kushusha bei vifaa vya ujenzi ilikuwa msaada zaidi kwa watu wa vijijini au mijini?

3.Prof.sera ya elimu bure ya mwaka 2010 ya CHADEMA ilikuwa rafiki zaidi kwa mwananchi wa kijijini au mjini?Na je kati ya Dr.Slaa na Kikwete ni nani alipata kura nyingi za vijijini?

4.Prof.kama watu wa vijijini ufisadi kwao ni issue,mwaka 2010 ni nani kati ya Dr.Slaa na Kikwete aliepata kura nyingi kutoka kwa watu wa vijinini?

4.Prof.unataka kuniambia kama Lowassa angepitishwa na CCM katika uchaguzi wa mwaka huu, watu wa vijijini wasingempaka kura kwasababu ya tuhuma za ufisadi zinazomkabili na badala yake wapiga kura wengi wa vijijini wangempigia kura mgombea wa UKAWA?

Prof. katika makala yako hiyo pia umezungumzia kile ulichokiita "ukigeugue wa karne" wa viongozi wa CHADEMA/UKAWA wa kumsema Lowassa kuwa ni fisadi na baadae kumtambulisha kuwa ni mkombozi wa Taifa hili kuwa ni moja ya sababu iliyowafanya watu vijijini kumkaa Lowassa.

5.Sawa.Sasa Prof. nikuulize.Viongozi wa CCM mwaka 2010 kusema kuwa elimu bure haiwezekani na kwamba viongozi wa CHADEMA ni waongo na mwaka 2015 viongozi hao hao wa CCM kuja na sera ya elimu bure.Je,huu si ukigeugeu?!

6.Prof. kwahiyo unataka kutuambia wananchi wa vijijini wanaona ukigeugeu wa viongozi wa CHADEMA tu na si ule wa viongozi wa CCM?

Prof. are you seriuos abaout this article?

I wonder!!
Prof anahulka kama Michael Wambura wa TFF, ni uzinguzi tu sijuwi kwa nini!
 
ACT wazalendo sera yao kuu ni kuiangamiza Chadema. Huyu anaandika makala kama mwana ACT-WAZALENDO na si Professor. Watu wa vijijini wanaishi kwa mazoea ufahamu wao ni mdogo matatizo yao yote njaa, ukame, umaskini, ujinga nk wanamsingizia Mungu wakati ni Man made yametengenezwa na watawala. Na mgombea wake wa ACT sababu ya kupata kura chache ni hizo hizo?
Pia usisahau wanaogopa vita kama Libya,Kuwait nk
 
Huyu ni mchumia tumbo siku lowasa anajiunga chadema alisema wamempata messi sijui alijua atashinda ili apate ulaji sasa wameiba kura akashindwa kageuka.
 
ACT wazalendo sera yao kuu ni kuiangamiza Chadema. Huyu anaandika makala kama mwana ACT-WAZALENDO na si Professor. Watu wa vijijini wanaishi kwa mazoea ufahamu wao ni mdogo matatizo yao yote njaa, ukame, umaskini, ujinga nk wanamsingizia Mungu wakati ni Man made yametengenezwa na watawala. Na mgombea wake wa ACT sababu ya kupata kura chache ni hizo hizo?
Sijui wataiua lini chadema maana mpaka sasa wana mbunge 1 akati chadema watakuwa na zaidi ya wabunge 70.
 
An empty stomach iz not a good political advisor. Hizo jitahada anazosema angekishaur chama chake
 
Back
Top Bottom