Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Ubungo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumza mara baada ya kupiga kura ya maoni leo Agosti 4, 2025 katika kituo kilichopo kwenye ukumbi wa Kibo Park uliopo Ubungo Kibo, ambapo amepongeza zoezi hilo akisema limefanyika kwa uwazi na demokrasia ya hali ya juu.