Prof. Ibrahim Haruna Lipumba for BoT governor | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba for BoT governor

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Nov 9, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mimi si mwana-CUF lakini leo nimemsikliza Prof. Lipumba wakti akihojiwa na Charles Hilary wa BBC Swahili hii jioni nimefurahishwa sana na jinsi jamaa alivyokuwa anajibu Maswali ya Charles na hoja za Wasikilizaji kwa uhakika na ufahamu mkubwa kuhusiana na mgogoro wa Kiuchumi unaozikumba nchi za Jumuia ya Ulaya. Huyu jamaa yuko juu na ndiyo maana IMF wamemchukua na alikuwa akihojiwa tokea Washington DC.

  Nina hakika kabisa kama Prof. Lipumba angelikuwa pale BOT uchumi wetu Tanzania ungelikuwa juu. Lakini kwa vile nchi hii imeshapoteza mwelekeo kutokana na utawala kwa kihuni wa CCM watu kama kina Lipumba wanapuuzwa simply because wako upinzani! Huu ni uhuni tu! CCM wameshindwa kujifunza kwa Nchi kama South Africa,USA, Uingereza na sasa Zambia kwa kutaja chache,kwamba Serikali zao zimeundwa kwa mchanganyiko wa Chama Tawala na Vyama pinzani kwa kujua umuhimu wa Uzalendo na kwamba nchi si ya Chama kilichoshinda kwa kura hata kama ni zaidi ya 50pc.

  Tunamshauri Kiwete aunde serikali ya mseto haraka sana kwa Tanzania Bara na awateue watu kama kina Prof. Lipumba kuwa Governor wa Benki Kuu badala ya Prof. ndullu anayeonekana kupwaya kwenye nafasi hiyo au kuwa Waziri wa Fedha badala ya Kibuyu Mustafa Mkullo. Pia kuna vijana matata wa CDM ambao wana ufahamu mkubwa sana wa maswala ya Kisiasa na Kiuchumi ambao kama Kiwete atawatumia ataondoka Madarakani akiwa amejijengea Legacy iliyotukuka!

  Siyo jambo la siri kuwa Prof.Lipumba yuko juu kwa mbali sana akilinganishwa na Prof. Ndulu au Mkulloi Hapa ni swala la kuweka uzalendo mbele na si ushabiki wa kisiasa wa kijinga unaoendeshwa na wanamagamba wa kufikiri kuwa Wapinzani ni wahaini ati wanataka kuipindua serikali iliyoko madarakani. Hayo nimmawazo ya ulimbukeni wa siasa, CCM lazima wakili kuwa nchi imewashinda na si vinginevyo. Lakini kwa vile sikio la kufa halisilkii dawa CCM acha wakomae na upumbavu wao,kwa sasa hawana siku nyingi za kuwemo madarakani maana ytayari taa nyekundu inayoonyesha EXIT inapiga indicator!!
   
 2. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,498
  Likes Received: 2,036
  Trophy Points: 280
  ndo unalijua leo hlo.!
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Talking is cheap. Huyu Professor alikuwa mshauri wakati wa Mwinyi with disastrous results.
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kama unajua tangu zamani mbona hujalisemea au kulipendekeza hapa ukumbini?
  Yale yale mambo ya kiswahili ya kulalamika vijiweni na kupiga domo. Jambo likItokea au likisemwa mara utasikia, oh,mimi nilijua tu...........itakuwa! Come on my friend,speak out your mind!
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Na CUF atamwachia nani?
   
 6. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  My friend FJM,

  Tofautisha kuwa mtendaji na kuwa mshauri. Unaweza kuwa mshauri mzuri lakini aliyeko kwenye nafasi ya utekelezaji akafanya kinyume cha kile ulichoshauri. Ndicho kilichotokea wakti wa Rais Mwinyi. Ushauri wa Prof. Lipumba haukuwa ukizingatiwa, Remember the same Prof. Lipumba wa hired by Yoweri Kaguta M7 to advice on Uganda's economy. Uganda economy propels with a supersonic speed when the Prof's ideas and advices were implemented accordingly.

  IMF wanajua nini Prof. Lipumba alifanya kwa Tanzania na Uganda na ndiyo maana wamemchukua yuko IMF Headquarters anakula kuku maana wanajua ni kichwa siyo mkia.
   
 7. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Huna hoja.

  Prof. Lipumba kwa sasa hivi yuko Washington DC kama mmoja wa maofisa washauri wa IMF, wewe unafikiri CUF kamwachia nani.
  Huko visiwani kuna serikali ya umoja wa Kitaifa, Katibu Mkuu wa CUF Maalimu Seif Sherrif Hamad ni Makamu wa Rais wa Zanziba ina maana naye nani kamwachia CUF??
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  JUzi ya Kiswahili nilisoma mawazo kama haya unayoyatoa hapa Makoye2009

  Cuf wataka serikali ya umoja wa kitaifa bara.

  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Serikali yatamalizwa kwa kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. CUF imesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeelemewa na majukumu ya kuongoza na hivyo kuhitaji msaada kwa kuundwa serikali hiyo kama ilivyo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, visiwani.

  "Baraza Kuu linaona njia pekee ya kulitoa taifa hapa tulipofikishwa ni kwa rais Jakaya Kikwete na CCM kukubali kusaidiwa dhamana ya kuongoza nchi kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Ali.

  Aliongeza kuwa hatua hiyo pia itaisaidia nchi kuvuka salama katika mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo itasaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo. Ali alisema serikali ya CCM imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuongeza kuwa tatizo la nishati hiyo linachangiwa na kuingizwa siasa na si utaalamu au rasilimali fedha.

  Cuf wataka serikali ya umoja wa kitaifa bara

  CCM na Serikali yao wanapewa ushauri mwingi tu ambao utaipesha TZ kuingia katika umwagaji damu lakini hawaonekani kuwa wanaona hatari inayolikabili taifa hili. Kwa hali inavyoendelea ya "maisha bora kwa kila mtanzania" na ubabaishaji unaofanywa wa kuleta katiba mpya au katiba viraka au kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi kuna dalili mbaya kwa siku zijazo.
   
 9. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160

  Unataka Kikwete aunde Serikali ya MSETO na CHADEMA waliokataa katu katu mambo ya serikali ya MSETO. Ni lazima wapinzani wenyewe waonyeshe kuwa wanaweza kushirikiana katika suala la maendeleo.

  Nafikiri mwenzangu hujawasikia CHADEMA wakati CUF wametoa wazo la MSETO bara. CHADEMA WALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWAZOMEA CUF eti kwa kuunda serikali ya Mseto ndio kidhibiti kuwa wao ni CCM B. Wakatupa matusi mpaka wakachoka.

  Mwenyewe angalia CHADEMA kama chama cha upinzani wanashindwa hata kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ndani ya bunge. Hawa hawataweza ushirikiano wowote ule kutokana na AJENDA ZAO ZA SIRI.
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Umeongea MKUU. Uko juu ya mstari, ON THE LINE. Thanks. VIVA JF.
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Mmabo matatu muhimu kwenye post yako>> moja nakubaliana na wewe kabisa kuwa Prf. Lipumba ni mchumi sio mwanasiasa so post yoyote ya kiuchumi akipewa anaweza kuwa potential kuliko hii ya kisiasa aliyo nayo. Pili governor sio post ya kisiasa, governor anaweza kuteuliwa mtu yoyote bila kujali chama chake lakini tatu katiba yetu hairuhusu serikali ya mseto kwa ushauri wako kwa rais hauzingatia matakwa ya kikatiba na mwisho kabisa usiwe mepesi sana ku conclude kwa kusikia tu kile mtu anachosema fanya utafiti kidogo juu ya utendaji wake kwani uzoefu unaonyesha ni rahisi sana kusema kuliko kutenda, things are easier said than done!!!
   
 12. ubun2

  ubun2 Senior Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The Governor of Bot is not the only one responsible for the state of the Tanzanian economy today. It is rumored that there are people at the BoT who have been looting Tanzania for the past 30 years. Those individuals are still there.
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Suala la uzalendo halimo katika kamusi ya watanzania wengi kwa sasa,kutofautiana itikadi za kisiasa hakumfanyi mtaalam wa fani fulani kuwa incompetent.Naamini katika mseto wa mawazo ili tuweze kujikwamua kutokana na huu umaskini unaoendelea kukithiri.Lakini kwa hali ilivyo sasa serikali inaonekana haiamini chochote toka kwa mtu aliyena itikadi tofauti na CCM kama yanaweza saidia..wacha tuendelee kupiga makitaimu..
   
 14. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata sasa JMKana team nzuri ya Uchumi watu kama Prof. Haji Semboja, ESRF team, Wangwe lakini uchumi ndio unadorora. Unayemshauri ana maamuzi mzuri hili ni swala la pili. I think Mr President hana priority ya kufufua na kusimamia uchumi. Huu ni mtazamo wangu tuu.  Nawasilisha.
   
 15. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mkuu unasema aunde serikali ya mseto ya Tanzania Bara!Kwani Tanzania bara ni nchi?Kwani yeye ni rais wa Tanzania Bara au Tanzania?
  Wewe haujui kuwa mkulu naye kasoma uchumi pale YUDIZIMU alafu ana phD!
   
 16. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Muongeaji mzuri sana mara nyingi sio mtendaji. Hayo mambo aliyoyaongea wengi wanayajua na walikosa nafasi ya kuulizwa kama alivyoipata yeye
   
 17. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Alipokuwa mshauri wa Mseveni alifanya vizuri sana
   
 18. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280

  Tatizo ni kwamba hata Lipumba akiwa Gavana ama Waziri Mkuu au hata Waziri wa Fedha hataweza kufanya chochote maana watawala ni wale wale wa CCM. CCM hawawezi muacha mtu afanye mambo kitaalam lazima wataingiza ufisadi, wizi, majunga na hata kumzuia asitekeleze wajibu wake kitaalam. Kama ni Lipumba kuwa Gavana asubiri hadi CCM wang'olewe ama na CUF au CHADEMA
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Makoye,

  Naomba ufafanuzi kidogo ni mwaka gani prof Lipumba alikuwa mshauri wa uchumi Uganda/M7 ?.Niliwahi kusikia mahali kwamba hii ilikuwa ni propaganda za kisiasa.


   
 20. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani hivi vitu vya uchambuzi wa kutumia natharia (theory) mtu kama ni mzuri wa kujieleza anaweza akateka dunia nzima, ila linapokuja swala la ku-fuse theory and practice, hapo ndipo kazi ipo na hapo ndio watu hupewa credit za ukweli...Mfano kuna mwana jamii moja katukumbusha kuwa Prof. alikua Lipumba alikua mshauri wa Rais Mwinyi ila mambo nayo hayakua mazuri..nae (Lipumba) alijitokeza wazi akasema sasa unaposhauri mambo mazuri alafu hayafanyiwi kazi, unategemea nini kitokee?? Mh. Godon Brown alie kuwa waziri mkuu wa wingereza, wengi walikua wakimsifu kuwa ni kichwa na angeweza kuingoza Wingereza vizuri, ili kilichompata enzi za uongozi wake kila mtu anakijua...Kwa mfumu huu wa serikali yetu hata akija DSK hakuna kitakacho badilika, kwasababu wataalamu wanashauri vizuri ila wanasiasa wanafanya vingine ili kujitajirisha wao na wala sio nchi.
   
Loading...