Prof.Euphrase Kezilahabi Mmh!

Domaradzka

Senior Member
Joined
Apr 19, 2016
Posts
135
Reaction score
168
Rais Kapera:
(Kwa uchovu) Hapa tulipo tumefika mbali. Hatuwezi kurudi nyuma. Tumepita katika misitu, majangwa na milima. Hatuwezi kurudi nyuma.

Waziri wa mambo wa nchi za Nje:
Hivyo ndivyo ilivyo. Mchumia juani hulia kivulini.

Waziri wa mambo ya ndani:
(Akidakia) Na mvumilivu hula mbivu.
(Kimya.Wanajikokota hatua chache. Sauti za watu waliao zinasikika nje ya jukwaa. Wanasimama kusikiliza)

Rais Kapera:
(Kwa sauti) Mnaolia huko, msitulilie sisi. Walilieni wajukuu wenu!
(Wananyamaza. Wanajikokota hatua chache)

Mkulima:
(Akinung'unika) Hii njia mnayonipitisha mimi siijui na mimi sijui mnanipeleka wapi!

Rais Kapera:
Mimi ndiyo dira yenu.Aniaminiye hatapotea njia.

Waziri wa mambo ya nje:
Hayo ni maneno yenye busara.Tunakuomba uwe kiongozi wetu wa maisha. Wewe ndiye haki. Wewe pekee ndiye unayeweza kufikiri.

Mkulima:
Hata hivyo nina haki ya kujua tunakokwenda, maana naona tunazunguka pale pale.Mimi mwenzenu nina mzigo mzito zaidi. Ninaumia sana!
( Kimya kwa hasira) Nijibuni ! La sivyo nitawakata na jembe!
( Mawaziri wanamshika.Waziri wa mambo ya nje anachomoa kisu ghafla)

Rais Kapera
( Kwa ukali) Rudisha kisu chako ndani ya ala ! ......



KAPTULA LA MARX ( Ukurasa wa 20)
 
Mtunzi wa vitabu mahiri kama Dunia Uwanja wa Fujo, Gamba la Nyoka, Rose Mistika nk. Kezilahabi yuko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…