Elections 2015 Prof. Benson Bana: Dk. Slaa ndiye pekee anayeweza kuitetemesha CCM

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,086
Habari wanabodi

Nyota ya Katibu mkuu wa CHADEMA inazidi kung'aa baada ya mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Proffesor Benson Bana kusema kwamba mwanasiasa mwenye nguvu kwa sasa anayeweza kuitetemesha CCM na hata kushika ikulu ni Mh,Dk W.P Slaa.

Ameyasema hayo wakati akihojiwa na Sauti ya America(VOA) jioni hii tarehe 22/07/2015..Amesema tafiti nyingi zinaonyesha Dk Slaa ana nguvu kubwa!

My take;
Nafikiri waliosema watashinda kwa goli la mkono wajiandae sana.
 
  • Thanks
Reactions: jme

Kwa kauli hiyo kibarua chake kimeingia mchanga
 
Si kweli...tafiti nyingi zimeonyesha Baba Yoyoo anaongoza...mchukueni huyo 👇
 
Attachments

  • 1437587647744.jpg
    1437587647744.jpg
    31.4 KB · Views: 558
CCM imeingiwa hofu, Magufuli kuwa shughuli

KUNA hofu imetanda ndani ya CCM; hofu ambayo inajaribu kufichwa mapema kwani kama mambo hayatobadilika ndani ya miezi hii mitatu hivi iliyobakia kabla ya Uchaguzi Mkuu basi chama hiki kikongwe zaidi nchini kinaweza kujikuta kikipumzishwa kutoka madarakani kwa nguvu. Dalili ya hofu hii imeonekana baada ya kutangazwa kwa mgombea wao wa kiti cha Urais Dk. John Pombe Magufuli.

Mojawapo ya mambo ambayo yametokea baada ya Magufuli kutangazwa ni kauli za kuwa yeye “anakubalika na anachagulika”. CCM imetaka kuliaminisha taifa kuwa Magufuli siyo tu anajulikana kwa utendaji kazi wake kwa kweli wananchi wengi wanampenda na wanaweza kumchagua. Kiasi kwamba wametaka watu waamini kuwa Magufuli ni Rais anayesubiria (President in waiting). Kwamba, upinzani hauna nafasi hata kidogo ya kumnyang’anya uwezekano huo.

Ukweli ni kuwa matendo ya CCM hayaoneshi kujiamini huku. Kama kweli CCM inaamini Magufuli anajulikana na kazi zake zinakubalika nchi nzima kwa nini juhudi kubwa sana inajaribu kufanywa ya “kumtambulisha”. Unamtambulisha vipi mtu ambaye tayari unaamini anajulikana, kufahamika na kukubalika? Ukiangalia utaona kuwa CCM inataka kumtumia Magufuli kukibeba chama; tatizo ni kuwa Magufuli mwenyewe – ukiondoa kukariri kwake takwimu mbalimbali – utendaji kazi wake una shaka.

Tayari wizara ambayo amekalia imeshagubikwa na kashfa lukuki na hili peke yake lingetosha hata kumchafua. Akija mgombea mzuri kutoka upinzani na akajizibu hizi takwimu za Magufuli, basi Magufuli na CCM iko matatani. Yote haya yanatosha kufanya watu wajiulize mara mbili kama kweli Magufuli hatokuwa shughuli kweli kweli.

CCM imepasuka, rekodi yake mbovu, na upinzani ukimsimamisha mgombea makini, Magufuli ataweza vipi kushinda? Njia pekee ya kushinda katika mazingira ya namna hiyo ni matumizi makubwa ya nguvu, vyombo vya dola na hata kuliingiza jeshi katika siasa kama walivyofanya chini ya Jenerali Shimbo mwaka 2010. Vyovyote vile ilivyo hata hivyo kuna hofu imetanda kwa CCM; hofu kama vile wingu zito la mvua lenye dalili ya radi na ngurumo. CCM hawajui sasa wafanye nini zaidi ya kuombea Magufuli aweze kuwaokoa. Akishindwa je Hili ndilo swali la kuogopesha zaidi kwa kila mwana CCM

Chanzo: Raia Mwema
 
Kuna uwezekano 300% muheshimiwa dr sla kuwa rais
Hiyo piga ua lakini lazima iwe
Na hilo limeandikwa duniani na mbinguni
 
Kwa hayo tunayoyaona na kuyasikia,basi Wanaumeee,Wanawakeeee,CCM,kwisha kwisha kabisa,nyang'anyang'a,mlalo wa chali,kifo cha mendeeee.
 
Back
Top Bottom