chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Dk Bana amesema jana kuwa Rais anatakiwa kuachwa afanye kazi yake ya kuongoza nchi na si kuvaa kofia nyingine ya kukiongoza chama na kutumia muda wa ziada kupambana na vyama vya upinzani.
Kikao hicho cha siku moja cha CCM kinatarajiwa kujadili masuala mbalimbali, yakiwamo makabidhiano hayo yatakayofanyika katika mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika mwezi ujao na kushuhudia Rais Magufuli akirithi mikoba ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete aliyemaliza muda wake wa uenyekiti wa chama hicho.
“Si lazima Kikwete aendelee na nafasi ya uenyekiti ingawa kafanya kazi nzuri. CCM ina watu wengi wazuri wanaoweza kushika nafasi hiyo na kukiongoza chama kwa mafanikio. Magufuli anapaswa kufanya kazi ya Serikali,” amesema Dk Bana.