Prof. Baregu ndani ya kipindi cha kipima joto ITV

Prof. Baregu ndani ya kipindi cha kipima joto ITV

ukisikia uzee dawa ndio huu prof kaelezea walivyomhoji karume na mambo mengi kuhusu kazi za tume ........sio kama wale simbilisi wa interahamwe....
 
Kuna kijamaa cha ccm kinaongea pimba sana hapa kuhusu muungano now itv..huyu jamaa ni mfanyakazi wa nida na aligombea kura za maoni na.dr kafumu igunga akashindwa..anaongea pimba tu
 
Ninamsikiliza kwa makini sana kweli Leo ITV wameweka watu makini!:thumbup:
 
Jamani Baregu kanikooooooshaaa,yani kama nipo Nkurumah anashusha lecture,huku mie nadesa kwa msela wangu Kayage......ssa ndio najua kwanini wajumbe wa katiba Intarahamwe walikataa wasiwe aehemu ya Bunge la Kutunga katiba mpya
 
Baregu kasema nn jamani tupeni mambo nasi tupate uhondo huo
 
Kuna kijamaa cha ccm kinaongea pimba sana hapa kuhusu muungano now itv..huyu jamaa ni mfanyakazi wa nida na aligombea kura za maoni na.dr kafumu igunga akashindwa..anaongea pimba tu


Huyo dogo kaniboa sana,,, afu anajitize ni mwanafunzi wa Prof. Baregu, mi nadhani Prof amemsamehe kumkataa huyo kilaza
 
Prof baregu amesema wamependekeza muundo wa 3 gvnt kutokana na mgogoro wa katiba ya zanzibar dhidi ya ile katiba ya muungano;anasema watawala wa muungano wamekaa kimyaa wakati katiba ya znz inavunja katiba ya jamhuri
 
I wish tungekua na watu/viongozi katika nchi hii wanaokuwa huru kufikiri na wanafikiri beyond their noses kama huyu Profesa!
Thanks Prof Baregu and thanx ITV kwa hicho kipindi
Tatizo nchi hii watu wamejaa UBINAFSI wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi na ndugu na jamaa zao!
Unakuta viongozi wakubwa tuu wengine wasomi wakubwa tu (at least kwa vyeti) lakini ukiwasikiliza ni kama watoto hivi yaani wanaongea mambo ya ajabu wanafanya analysis na comparisons za kitoto kwelikweli
 
Mzee Prof. Baregu kaongezea zege kwenye msimamo wangu. Jamani kwa kweli CCM wanakotupeleka siyo kabisa. Na hofu yao kumbe ni kukosa majimbo. Kudadeki. Kura ya maoni lazima nikapige tu.
 
Mbona hamuelezi alichosema hata cc tuliokuwa mbali na tv tupate elimu?! nzishe zenu.
 
Jamani sisi kwetu umeme umekatika wakati anaongea kijana mwenye kipara. Nilikuwa na shauku sana ya kipindi Tanesco wamenikatili. Pse eleza mjadala uko vipi nani kangaa Zaidi hapo
 
Prof baregu amesema wamependekeza muundo wa 3 gvnt kutokana na mgogoro wa katiba ya zanzibar dhidi ya ile katiba ya muungano;anasema watawala wa muungano wamekaa kimyaa wakati katiba ya znz inavunja katiba ya jamhuri
Hii kasema tu kama mfano ulio hai na mojawapo ya kero na hatari ya uhai wa Muungano wetu.
Ila kasema tatizo (dalili za ugonjwa) kubwa lililopo katika Muungano wetu (ugonjwa wenyewe) ni muundo mbovu tulio nao
na kwamba Yeye kama Yeye angependa Muundo wa Serika moja (sio kwa sababu ya gharama ila kuimarisha Muungano)
ila hakupata wafuasi wengi na kubwa zaidi ni kwamba sheria iliwakataza kupendekeza serikali moja hata kama wananchi wengi wangependa hivyo..coz sheria ilisema Lazima uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar uzingatiwe!
 
prof baregu akichambua rasmu ya katiba ambayo yeye alikuwa ni mjumbe wa katiba. Kasema viongozi wa tz ni wanafiki, watu wanaopenda kujipendekza na kuacha uongo utawale. Kasema kinachofanyika kwa sasa ni kuchochea wananchi waichukie tume. Kama machafuko yatakuja apa nchini kasema wale wanaopinga maoni ya wananchi basi watabeba lawama hii chama tawala na serikali yake. Kila mtu anataka maoni yake yawemo kwenye katiba, lakini ata yeye aliyekuwa kwenye tume, maoni yake hayakuingizwa baada ya mchakato mzito. Mwisho kasema bunge maalumu la katiba limeenda kuidhinisha matakwa ya wananchi na si kutengua kile walichopendekeza waananchi. Nimetafuta line ili nimuulize prof baregu, je mh. Dr mwakyembe na prof shivji wako sawa kulingana na taaluma yao kwamba wanapendekeza serikali 2?
 
Wasomi kama prof baregu ndio wanafaa kupew nafasi za uongozi ku replace wale wanao kwenda kanisani
 
Back
Top Bottom