Sio ajabu Baregu ni mlokole zaidi ya walokole wengine wanaojipigia debe, Mungu huangalia moyo wa mtu, hayumbishwi na mitazamo ya watu. Kama sivyo, Daudi asingepakwa mafuta kuwa Mfalme wa Israel mtoto mdogo asiyetarajiwa; Sauli (soma Paulo) asingekuwa mpiga debe maarufu wa Yesu Kristo hata kuwazidi mitume wengi waliotembea na Yesu miaka mitatu mfululizo. Mungu huwainua wangyone na kuwashusha wenye viburi. Nikodemus pamoja na kuwa msomi wa Kisamaria, alilazimika kutambua kwamba pamoja na kujulikana sana machoni pa watu kama mcha Mungu hakuwa na kitu, akalazimika kumwendeaYesu Usiku kula shule namna ya kuingia Mbinguni, Mungu akamkweza sana hata leo tunasoma habari zake. Yusufu ambaye hakutambuliwa na watu kama mwanafunzi wa Yesu akawa ndiye msaada wa kubeba msalaba wa Yesu kuelekea Golgotha wakati waliojulikana waliingia mitini.
Debe tupu mara zote haliachi kutika, Ngombale Mwiru amesemwa kwamba hana dini - ni makosa kusema hivyo, kwa sababu anayo dini ya mababu zake inayomtia nguvu kuwa mtu anayeishi na watu katika principles za imani ya dini yake. Neno zuri tuseme Baregu sio mkristo, hakuna dini ya kipagani. Waebrania waliwasema wasioamini kama wao "pagan", kama wachaga wanavyowaita "Kyasaka" wenzao na wanyakyusa wanavyowaita wenzao "Bhajanga", na wakinga huita "Bhanng'alu"..... Wapagani ni watu wasiokuwa na dini inayofanana na unayoiamini wewe. Kama ni kwa namna hiyo, basi tumtendee haki Baregu. Mbona ni mpole kupindukia na Mungu anapenda watu wapole? Ni mtu wa Mungu yule kama alivyo Mwislam, Mhindu, Myahudi, Mkristo, Budha na kadhalika.