Prof. Baregu aula SAUT

Andindile

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2009
Posts
304
Reaction score
19
Hatimaye professor Mwesiga Baregu amesaini mkataba na chuo kikuu cha mtakatifu Augustino baada ya kuzuiliwa na serikali kufundisha chuo kikuu Dar. Habari za ajira yake zimethibitishwa na Mkuu wa idara ya Mawasiliano ya Umma wa SAUT Padri Dr. Joseph Matumaini kwenye gazeti la Tumaini letu toleo la Ijumaa, Feb. 19-25, 2010. Dr. Tumaini amesema kuwa ajira yake ni ya mkataba wa miaka mitatu na unaweza kupitiwa upya kila umalizikapo. Atakuwa anafundisha kampasi ya Dar es salaam na Mwanza. Natumai Prof. ataendeleza imani yake katika uhuru wa kitaaluma huko aliko na atakuwa kichocheo cha taaluma SAUT na ikizingatiwa kuwa SAUT kimekuwa chuo cha kwanza Tanzania kuanza kutoa shahada za uzamili na uzamivu katika tasnia ya habari na mawasiliano ambako uhuru wa kutoa habari ni jambo la msingi sana. Namtakia mafanikio mema Prof. Baregu
 
Naimani safari hii baada ya adhabu ya UDSM, atafuata sheria na code of conduct!
 
Bado mwampandikia choko choko tu kila anakokwenda?


Huyu si ndie yule aliekataliwa mkataba UDSM? Mtu kama yeye profesa anatakiwa asome mikataba anayo sign, huyu jamaa alifanya mambo against his contract, haya ni makosa, angekuwa nchi yoyote hukumu ingekuwa hiyohiyo

Alionyesha udhaifu zaidi pale alipo jitetea kwa kusema, wako wengi wamefanya makosa kama yeye!! huu kwa kweli ni utetezi wa kidhaifu hasa kwa mtu mwenye jina la PHD kama yeye

Haina maana mwizi akiiba na wewe uko na haki ya kuiba, Ethical na code of conduct lazima uifuate no matter what!!
 
Kama sheria inasema hivyo, mbona sasa jamaa kaajiriwa kwa kazi ileile na huku ni Mwana siasa? Ngoja uchaguzi ujao tutaona watu wanavyopelekana mahakani mara wakishindwa.

Wee Bull, hii sheria ikipitiwa kikweli kweli basi wengi watalia. Kitendo cha Rais kuwa mwenyekiti wa CCM/Chadema, CUF ni uvunjaji wa sheria hiyohiyo ambayo Baregu kakataliwa kufundisha UDSM. Kibaya zaidi ni kuwa wanaokomolewa ni watoto wa Masikini kwa kukosa kufundishwa na Mzee/mwalimu mwenye uzoefu wa hali ya juu. tatizo la waalimu vijana ni kuwa hata mifano yao huwa imekaa kiujana ujana. Mzee kama huyu akikupa somo na akakupa mifano halisi, somo linakuingia utafikiri umepigwa lile lisindano la PPF!!!

Ukiona nchi kama hii na utendaji huu, unaona heri tu nichukue Uraia wa Rwanda haraka.
 
Wabongo bado tuna ukoko wa utamaduni wa kuona mtu aliyepata kazi "kaula"?
Utafikiri mtu kashinda bahati nasibu ya mabilioni!

Nafikiri subconsciously tunaona sehemu ya kazi ni sehemu ya "kula" na wala si ya kutumika. No wonder vita dhidi ya ufisadi ngumu, wananchi wenyewe wanategemea kila mtu "ale" sehemu ya kazi yake.

Unaweza kusema ni maneno tu, lakini Freud angekwambia maneno yana jinsi ya kufunua watu wanavyofikiri deep inside their heads.

Pathetic.
 
Hizi ni habari njema.Baadaye nitampigia simu kumpongeza.Am very happy for him.MUNGU hatumpi mja wake.
 
Hizi ni habari njema.Baadaye nitampigia simu kumpongeza.Am very happy for him.MUNGU hatumpi mja wake.

Kwa taarifa yako Prof. Baregu haamini kama kuna MUNGU. He is totally a pagan. Hii inasikitisha sana. MUNGU amsaidie ili atambue ya kuwa yuko MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake.
 
Kwa taarifa yako Prof. Baregu haamini kama kuna MUNGU. He is totally a pagan. Hii inasikitisha sana. MUNGU amsaidie ili atambue ya kuwa yuko MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake.
sasa hapo ndipo mnapokosea, wewe thibitisha UUNGU wa MUNGU wako, kwa Baregu wewe pia ni mpagan, kwani lazima Uabudu kwa Mungu wa mashariki ya kati ? yeye anaamini Mungu wake anaeishi kule Kagera , kwenye pango fulani, sasa wewe endelea na Kumtusi, kisha utashangaa Baregu anaenda kwa mola wake, na wewe unaulizwa, kwanini ulimtumikia Mungu wa mashariki ya kati, wakati kila taifa, kila mkoa, kila kijiji, kila kaya , inaMungu wake....Miungu yetu si ushenzi........mmepoto, mmepotosheka, mjiandalie jehanam, shauri yenu.
 

CCM mpo???
 

Sijaona mahali panaposema Mungu hawapendi wapagani. Kwa taarifa tu, Mungu anahangaikia kuwapata wapagani kuliko wale alio nao tayari, kama konda anavyohangaika kuwaingiza abiria walioko nje ya daldala yake kuliko wale alio nao ndani tayari. Ukibisha mwombe konda akushushie kituo cha msaada kama hakuna abiria anayengojea gari hapo. Mwache Baregu apate kilicho chake, hakuna ajuaye Mungu anayo makusudi gani juu ya Baregu.
 
Le'njobe dhana ya Mungu na UUNGU , inatofauti sana , kwa jamii moja na nyingine, Ubora wa Mungu unategemea wewe unaabudu nini, ushenzi kwenye Imani unalalia kwenye dhana ya huyu si wetu, ama mwenzetu. ila kwa ujumla wake, Muhindu akiwatazama Waislamu ama Wakristo anaona viumbe dhalili, visivyomjua Mungu wa kweli, dhana hiyo anayo Muislamu dhidi ya dini za wengine vilevile Kwa Wakristo wao wanawaona wengine kuwa wanaabudu Miungu ilhali imeandikwa ...."mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu...."
sasa Ukiitazama Falsafa hiyo hakuna aliesahihi kumuhukumu mwenzake, maana hata yeye umzaniae amepotoka anakuona wewe , au sisi kuwa tuumepotoka kabisa.
 
namwamini sana huyu jamaa kwa kuwa kwenye fundisha yake huwezi lala kama za maprof wengine.nasema ivi kwa kuwa nimebahatika kuwa mwanafunzi wake kwa semister mbili.Mungu ambariki
 
Kwa taarifa yako Prof. Baregu haamini kama kuna MUNGU. He is totally a pagan. Hii inasikitisha sana. MUNGU amsaidie ili atambue ya kuwa yuko MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake.
Hivi ni kweli? kama ni kweli, basi, usemi usemao, kusoma kwingi uondoa mahalifa, ni sahihi
 
Hivi ni kweli? kama ni kweli, basi, usemi usemao, kusoma kwingi uondoa mahalifa, ni sahihi
kipo anachokiamini, lakini haamnini katika Mungu wa aina ya Waislamu, Wakristo ama Wahindu....?
 

Tunakutakia mafanikio mema mpambanaji
 
Mungu huwapenda watu wote, ndo maana huwanyeshea mvua watu wote, wema na wabaya. Hiyo nayo ni mvua ya baraka kwa Prof Baregu. Kutokuamini kuwa Mungu yupo sidhani kama ni vibaya,its a matter of time. iko siku ataamini na kubatizwwa na kuokoka... kama biblia isemavyo...
 
a different opinion is good when there is one to be different from, or is it not?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…