Prof. Baregu aanza kazi SAUT


P

Paschal Matubi

Senior Member
Joined
Sep 15, 2008
Messages
114
Likes
56
Points
45
P

Paschal Matubi

Senior Member
Joined Sep 15, 2008
114 56 45
**********************************************************

Waweza kusoma habari hii hapa chini au attachment niliyoambatanisha humu ambayo ni scan ya gazeti la TUMAINI LETU.

**********************************************************

{Prof. Baregu aanza kazi SAUT}

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (SAUT) kinachomilkiwa na Kanisa Katoliki nchini kimeingia mkataba na Profesa Mwesiga Baregu ambapo atafundisha katika chuo hicho kulingana na mkataba huo.

Hatua hiyo ya Profesa Baregu kujiunga na SAUT inkauja baada ya suala lake na Chuo Kikuu cha D'Salaam kumalizika na kwamba ujio wa profesa huyo unaleta changamoto katika maendeleo ya taaluma ya uandishi wa habari na mawasiliano nchini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa Profesa Baregu tayari amekwishaanza kufundisha katika kampasi ya D'Salaam ya SAUT ambako kuna wanafunzi wa shahada ya uzamili (MA) na uzamivu (PhD).

Akizungumza na TUMAINI LETU kwa njia ya simu, mkuu wa idara ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Padri (Dk.) Joseph Matumaini alithibitisha tarifa hiyo na kwamba tayari wameingia mkataba na Profesa Baregu na atakuwa akifundisha katika kampasi ya D'Salaam na Mwanza yaliko makao makuu ya SAUT.

Dk. (Padri) Matumaini alisema kuwa kuwepo kwa profesa huyo hapo chuoni SAUT kunaleta matumaini mapya na changamoto katika tasnia ya habari kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika fani mbalimbali kitaaluma.

"Ni kweli Prof. Baregu amekwishaanza kazi SAUT kwa sababu tunatambua mchango wake na tunaamini ataongeza nguvu katika kukiimarisha chuo chetu katika utoaji wa elimu bora", alisema Dk. (Padri) Matumaini ambaye pia ni mhadhiri katika chuo hicho.

Alifahamisha kuwa ni matumaini ya SAUT kuwa Profesa huyo atatumia uwezo na ujuzi wake kitaaluma kuwanufaisha wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kinacholenga kuleta mapinduzi ya tasnia ya habari na mawasiliano ya umma nchini.

"Sisi tunafahau kuwa Profesa bareu ana mchango mkubwa sana kitaaluma, hivyo tunategemea tutabadilishana naye mawazo kitaaluma katika nyanja tofauti ili kusaidia utoaji wa elimu ukizingatia kwamba chuoa chetu ni ca kwanza kutoa shahada ya uzamili na uzamivu katika tasnia ya habari na mawasiliano", alisisitiza Dk. (Padri) Matumaini.

Alifahamisha kuwa mkataba alioingia profesa huyo ni wa miaka mitatu ambao hata hivyo unaweza kupitiwa upya kila unapomalizika.

**********************************************************
Chanzo: Gazeti la TUMAINI LETU
Mmiliki wa gazeti: Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la D'Salaam
Toleo la Gazeti: Namba 00298, February 19, 2010
Sehemu ya Gazeti yenye habari: Ukurasa wa 04

**********************************************************
 

Attachments:

Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
12,057
Likes
1,424
Points
280
Zogwale

Zogwale

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
12,057 1,424 280
Safi sana, acha SAUT wamtumie mwanazuoni huyo mahiri. Ila tu Prof. Baregu utulie uheshimu kazi yako, shughuli binafsi na zile za kisiasa zisimeze (outweight) vipindi vyako. Hongera, tunategemea matunda mazuri ya kazi.
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
27,790
Likes
31,946
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
27,790 31,946 280
Safi sana, aachane na wakina Hawa Ghasia wasiojua faida ya Wahadhiri wetu na uhaba tulio nao
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
. Ila tu Prof. Baregu utulie uheshimu kazi yako, shughuli binafsi na zile za kisiasa zisimeze (outweight) vipindi vyako. Hongera, tunategemea matunda mazuri ya kazi.
unachosahau ni sawa na kile ambacho serikali imejisahau kuwa Prof.Baregu ili abaki kuwa mwalimu mzuri ni lazima ajishughulishe na siasa kiundani hasa, maana yeye amebobea ktk siasa , na anawafunza watoto wetu siasa, hivyo lazima awe muelewa kiasi cha kutoosha.
ni sawa na bwana shamba asie na shamba, anaonekana kupwaya mbele ya macho ya Pinda[PM]
vilevile ni sawa na kina Prof Shaba , ingawa yeye ni daktari wa kuchunguza maiti na amekuwa mwalimu pale Muhimbili UNiversity kwa miaka zaidi ya 25,
elimu ya chuo kikuu inahitaji watu waliobobea hasa, sasa utabobeaje kama utendi kile ambacho taaluma yako inakutaka utende.?
kumbuka chuma kisichotumika huota kutu kwa kasi....
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Safi sana, acha SAUT wamtumie mwanazuoni huyo mahiri. Ila tu Prof. Baregu utulie uheshimu kazi yako, shughuli binafsi na zile za kisiasa zisimeze (outweight) vipindi vyako. Hongera, tunategemea matunda mazuri ya kazi.
Yeye ni mwalimu wa siasa ataachaje siasa Prof. Baregu na siasa ni kama chanda na kidole havitenganishwi kwa urahisi.
 
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,525
Likes
8
Points
135
Josh Michael

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,525 8 135
Wote ni Watanzania na kazi ya SAUT ni nzuri sana katika ujenzi wa Taifa letu, hivyo kwa Prof Baregu anaweza kuwa chachu ya wanafunzi kubwa sana
 
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Messages
1,315
Likes
115
Points
160
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2009
1,315 115 160
Ila tu Prof. Baregu utulie uheshimu kazi yako, shughuli binafsi na zile za kisiasa zisimeze (outweight) vipindi vyako.
SAUT waliomchukua walisema mapema kabisa kwamba wanajua Prof. Baregu ni mwanasiasa na wanajua haitamzuia kutoa elimu yake pale. Kumbuka ilitamkwa vile siku mbili tu UDSM walivyomtupa Baregu kwa kujidhani bado ni chuo cha kubabaikiwa na kunyenyekewa kana kwamba utandawazi haujakifunika kwa kuleta vyuo vikuu tele.

Wewe Maane ungekuwa unamiliki University yako basi ungesubiri Baregu aje kuomba kazi kwako na umueleza hiyo kauli yako ambayo naamimi Baregu angeachana na wewe kabla hujamalizia sentensi yako. Hata mimi ukinieleza hayo sina haja ya kunyenyekea kufundisha au hata kusoma katika chuo chako!
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
Wote ni Watanzania na kazi ya SAUT ni nzuri sana katika ujenzi wa Taifa letu, hivyo kwa Prof Baregu anaweza kuwa chachu ya wanafunzi kubwa sana
ni kweli Josh, SAUT inaweza kutoa funzo kwa watendaji dhalili wa sekta za umma,
mimi naamini SAUT wamelamba dume kwa kupata hicho kichwa na inaweza ikawaongezea hadhi na heshima.
 

Forum statistics

Threads 1,251,231
Members 481,615
Posts 29,763,388