Problem ya Samsung flat screen

Problem ya Samsung flat screen

tofali

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
4,010
Reaction score
3,423
Habari wana jamvi..mm nilinunua katv haka ka 22" kwa ajili ya chumbani...nilikanunua mwezi wa 11 mwaka 2011ghafla mwaka 2012 julai kakagoma kuonyesha...bahati mbaya sina warrant...tatizo lake ni kuwa kanaongea lkn picha screen ni whit tupu....halafu nakapenda mno...nilikwenda Samsung freedom electronic pale jmall nikaambiwa eti kameingia maji kwa hiyo inabidi niwekewe screen nyingine..bei ya screen ni laki2 na bado ufundi..aisee nilichoka..nikakaweka uvunguni nikaamua kwenda kununua tv ya kichogo mpya ya Samsung nikaweka chumbani...ila sasa ni mwaka tv yangu naionea huruma kukaa uvunguni...nisaidieni niende kwa fundi gani.?...na je bei ya screen mpya ndo hiyo? Na ufundi bei gani maana nilivyopiga hesabu km screen ni laki2 na ufundi bado si itafika lk 3...ndio maana nikaamua kwenda kununua mpya cz niliogopa nisije tupa hela halafu wakaniwekea kioo used..mwsho wa siku kiniharibikie...msaada mwenye kujua nifanyeje
 
Watanitafuta wengi..ni bora aseme wazi ili wenye shida km yangu nao wafaidike...aelekeze aliko..biashara matangazo
 
Flat screen LCD LED PLASMA au aina gani?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Du Pole Sana. Mm pia nlinunua Samsung TV kwa Agent wao Karikoo, baada tu ya Warrant yangu kuisha,haikupita Miezi Miwili TV ikapitisha Mstari katikati kwenye kioo na Kugawanyisha Picha.

Nlivyowapelekea Pale JMall Samsung Service Centre, Wakanambia kioo kimekufa, na kwa vile Warrant imekwisha ntalazimika kuwalipa 550,000 ili waniwekee Kioo kingine.

Nlichokifanya laki tano na nusu hiyo nkaongezea hapo tano nyingine nikanunua 40' Inch LED Smart TV Series 6.

Saiv natafuta kioo Used ili niweze kubadilisha kwenye ile ilokufa ambayo ni 32 Inch kisha nii uzilie Mbali.

Mwenye nacho Kioo cha Samsung LCD 32 Inch ani PM tufanye Biashara.
 
Aiseee pole sana...me nahisi hawajakaa sawa kwa utaalamu hawa samsung...sidhan km sony zinasumbua hivi...halafu nilikuja sikia eti kale katv kangu zilikuwa ndo product zilizokuja mbovu..ila waliokua na warrant walikua wanabadilishiwa na kupewa mpya cz samsung wenyewe waligundua ni mbovu.so ht mimi ningekua na warrant ningebadilishiwa..alinitonya mfanyakazi wao
 
Kwa case hizo mbili ni mapema sana kusema ni tatizo. Yawezekana ni defaults za kawaida za electronic devices sababu waliwapa warranty traditionally maana yake ni kuwa wanajiamini ladda kama zina life span hivyo wanajua baada ya mwaka zitasumbua amabayo sidhani kwa muwekezaji mwenye jina kama hilo anaweza kukubali kujikwamisha kizembe kiasi hicho

I have one since 2010 na inafanya kazi vizuri tena resolution ni safi kuliko sony(ambayo natumia mimi)

Mlipokwenda waliwaaambia chanzo ni nini,maana uliambiwa imengia maji na hujakanusha sasa kama kweli hapo wa kulaumiwa ni nani??!!!

Kwa wataalamu watujuze matatizo hayo husababishwa na nini maana hata kwenye laptops huwa yanatokea
 
Watanitafuta wengi..ni bora aseme wazi ili wenye shida km yangu nao wafaidike...aelekeze aliko..biashara matangazo

Uko sahihi mkuu, mimi pia nilipatwa na tatizo kama hilo kwa TV yangu LG 29" nayo inaonekana yaliingia maji na inaongea lakini picha hakuna, hadi leo ni kama mwaka na nusu sasa sijapata spare (wanaiita IC). Niliamua kununua nyingine (this time Samsung 42") ambayo ninayo hadi leo kutoka wakati huo, lakini bado hii LG nahangaikia ipone. Hivyo kwa uzi huu tunaweza tukapata faida wengi.
 
Kwa case hizo mbili ni mapema sana kusema ni tatizo. Yawezekana ni defaults za kawaida za electronic devices sababu waliwapa warranty traditionally maana yake ni kuwa wanajiamini ladda kama zina life span hivyo wanajua baada ya mwaka zitasumbua amabayo sidhani kwa muwekezaji mwenye jina kama hilo anaweza kukubali kujikwamisha kizembe kiasi hicho

I have one since 2010 na inafanya kazi vizuri tena resolution ni safi kuliko sony(ambayo natumia mimi)

Mlipokwenda waliwaaambia chanzo ni nini,maana uliambiwa imengia maji na hujakanusha sasa kama kweli hapo wa kulaumiwa ni nani??!!!

Kwa wataalamu watujuze matatizo hayo husababishwa na nini maana hata kwenye laptops huwa yanatokea

Ndugu yangu maji hayo yaliingia saa ngapi.?? Nyumba haivuji...ni tv tena ya room naitumia mwenyewe..nilipigwa na butwaa tu..cz waling'ang.'ana ni maji...basi ni kasema ok isiwe tabu...sasa kuna kijana namfahamu anafanya kz pale akaniambia hiyo product yako zilikuja gundulika kuwa zinashida..so Samsung wenyewe ikawa mtu akija kuleta atengenezewe alikua anapewa mpya kabla warrant haijaisha..kwahyo na mm ningekua na warrant labda ningebadilishiwa cz wengi walirudi walionunua 22" kipindi kile
 
just PM me nipo Dar ni kweli vioo vya flat ni ghali kwani kuvipakia kwenye ndege ni bima kubwa.but tuwasiliane kwaani pia vipo used
 
Samsung lcd nyingi zinasumbua vio.Namara nyingi huwa haviingiliani.Mwambie fundi akuangalizie zile taa za ndani ya tv.Mda mwingine huwa zinakufa.Au vot zinazo enda kuwasha taa hazitoki.Nakushaul mwone fundi tv mzuri atakupa jibu sahihi.
 
Kama ulinunua Kariakoo umelizwa kwa sababu Kariakoo na maduka mengi wanauza Samsung na TV flats aina nyingine feki,huku nje ni Samsung lakini ndani ni mwenyekiti Mao Tse Tung,siku nyingine ununue kwenye maduka maalumu ya makampuni hayo kama jamaa wa Samsung pale JM Mall,Kisutu na Mlimani na hakikisha unapata warrant ,mara nyingi inakuwa si chini ya mwaka,hata Game wanauza vitu halisia na hutoa warrant
 
@ mfianchi tv nilinunua jmall fredoom electronics...tena ndio maagent wa samsung tanzania....
 
LCD, LED na PLASMA tvs' zinaitaji matunzo ya hali ya juu, haziitaji mtikisiko mkubwa, iweke sehemu ambayo haitaweza kuguswa au kugongwa na kitu kingine hasa Kwenye Kioo. isiwekwe kenye meza ambayo ikiguswa inaweza kutikisika kwa urahisi na kusababisha TV yako kupata mtikisiko au kujigonga Sehemu nyingine hasa kwenye Frame/Panel inayoshika kioo/Screen.
 
Habari wana jamvi..mm nilinunua katv haka ka 22" kwa ajili ya chumbani...nilikanunua mwezi wa 11 mwaka 2011ghafla mwaka 2012 julai kakagoma kuonyesha...bahati mbaya sina warrant...tatizo lake ni kuwa kanaongea lkn picha screen ni whit tupu....halafu nakapenda mno...nilikwenda Samsung freedom electronic pale jmall nikaambiwa eti kameingia maji kwa hiyo inabidi niwekewe screen nyingine..bei ya screen ni laki2 na bado ufundi..aisee nilichoka..nikakaweka uvunguni nikaamua kwenda kununua tv ya kichogo mpya ya Samsung nikaweka chumbani...ila sasa ni mwaka tv yangu naionea huruma kukaa uvunguni...nisaidieni niende kwa fundi gani.?...na je bei ya screen mpya ndo hiyo? Na ufundi bei gani maana nilivyopiga hesabu km screen ni laki2 na ufundi bado si itafika lk 3...ndio maana nikaamua kwenda kununua mpya cz niliogopa nisije tupa hela halafu wakaniwekea kioo used..mwsho wa siku kiniharibikie...msaada mwenye kujua nifanyeje

Mimi namjua fundi mzuri sana kwa tatizo hilo gharama yake ni sh laki tatu tuu.
 
kwahiyo wadau ni aina gani ambayo ni nzuri ili sisi ambao tunataka kuzitafuta kwa mara ya kwanza tusije tukaingia mkenge?
 
Aisee mm flat ya sumsung 34" mtumba nilitumia miezi 2 tu ikabadilisha picha updown side na picha zinakuwa chenga chenga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom