Pro.Maghembe Mradi was maji kutoka Kirya kwenda Same na Korogwe umeishia wapi??

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,103
Sikutarajia jipya kwenye serikali ya Maghufuli kwenye Wizara, yaani anateua watu ambao chama chake kilisimama na kusema ni mizigo yeye ndiyo anaona ni Safi, Kuna Mtu anaitwa prof.Maghembe alikuwa waziri wa maji na anajua kabisa kuwa alishindwa kuisimamia miradi mikubwa ya maji kama Mradi unaotoka kwenye Bwawa la nyumba ya Mungu kata ya Kirya kuja Mwanga maeneo ya Kiverenge kisha same na Korogwe, Mradi huwo kwasasa umesimama.

Kuna mradi wa Ruvu kwaajili ya Dar es salaam ila kila mmoja anajua mradi huwo unavyokwenda, yote haya na mengine mengi yalikuwa chini ya huyu bwana lakini Hamna kitu.

Jimbo analotokea Bwana huyo wakazi wake zaidi ya 90% hawana maji safi na salama ya kunywa,Miundombinu ni mibovu sana, Mfano maeneo ya Kilomeni na Ngujini ni kama vile ni visiwa vya nchi kavu ila sijawahi kumsikia mbunge huyu akizisemea Changamoto hizi mahala popote pale,iwe kwenye Bunge ama vikao vya madiwani.

Kuna maeneo ya mipakani kama vile Kata ya jipe,Kigonigoni Toloha nk. Niliwahi kupeleka swali bungeni kupitia Kambi Rasmi ya upinzani juu ya Mateso na manyanyaso wanaopitia Wananchi hawo wanaoishi kando kando ya ziwa jipe kwa kukamatwa wakati wakivua Samaki na kupelekwa nchi jirani wengine kufungwa na wengine kuombwa rushwa..... Ila mbunge wa jimbo husika alikuwa kimya kana kwamba jimboni kwake hali ni shwari.

Nashukuru niliingia kwenye mapambano nimemaliza salama, nimezidi kuimarika nimekuwa imara zaidi ya Jana,japo wananchi wangu wa Mwanga wanaumia na kusononeka kwa kilichotokea, Nimeamua kuchora mstari,Nimeanza pambano upya nikiwa imara zaidi.

Tusihofu pambano LA 2016-2020 Litakuwa nitakatifu sana Halina kikomo wala wa kujaribu kulizuia.

Namshukuru mungu ni mzima, nawapenda wote na nnawatakia nyote sikukuu njema.... Karibuni kwenye mapambano Mapya 2016-2020 Mwanga.

Henry Kilewo
Never Say Never
 
Watanzania bwana - twambie kama personal issues na Prof!!! Imekuwaje unahibuwa madai/shutuma baada ya kusikia Prof.Maghembe kateuliwa kwenye wadhifa wa Uwaziri unakuja na stori zako za udaku ukiwa na lengo la kumchafua Mzee wa watu,sijui anasumbuliwa na kitu gani: roho ya kwa nini,wivu au plain sadism?
 
Usicheze na maghembe, mafebrruary,na lwengesi .waganga wakutoka Gambia naona wamewafanyia kazi yao vizuri kwani licha ya kuwa waliacahwa na mh magufuri lakini mwishowe mambo yamekuwa bora kabisa
 
Back
Top Bottom