Clemence Mwandambo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2018
- 1,384
- 1,438
Siku moja katika matembezi yangu mida ya Jioni wakati napita kandoni mwa barabara eneo la raundi about kama tulivyozoea kupaita hapa Mbeya mjini nikielekea maeneo ya Uzunguni, nilimuona kichaa Mzee akiwa na mkoba wake mchafumchafu.
Nilimsogelea mahali alipokuwa ameketi alinitazama kwa macho makali mpaka niliogopa. Wakati naanza kujihami ili niondoke aliniita akaniambia keti dogo wala usiogope.
Nilimsogelea, akaniambia dogo nikuambie kitu, nilimuitikia kwa kichwa nikiashiria kukubali. Akasema dogo you know this country is prison? Nikamuuliza why? Nikamsogelea zaidi. Akasema dogo hii nchi ni gereza, na mkuu wa nchi ni mkuu wa gereza, na wale wa chini yake ni manyapara, kwa hiyo usitegemee mkuu wa gereza kuleta maendeleo gerezani.
Kazi ya kuu wa gereza ni kudhibiti wafungwa, na sio kuleta maendeleo gerezani. Kipindi hicho kilikuwa kikwete akiwa rais wa nchi awamu ya kwanza. Akaniambia dogo hata gerezani kuna wafungwa wenye maisha nafuu na wengine maisha mabaya.
Mwisho akaniambia dogo hakuna nchi iliyowahi pata uhuru kwa amani, uhuru haupewi mezani, akabeba mkoba wake akasimama na kuniambia hii nchi ya malikia dogo. Bado TUKO chini ya mwingereza. Akaondoka na kuniacha NIKIWA nimeketi.