Principles za mahusiano yanayodumu

Principles za mahusiano yanayodumu

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,119
Katika siku za karibuni kumekuwa na posts za watu mbalimbali ambazo mara nyingi huwa zinaonyesha migogoro kuanzia kwenye simu. Sasa ntajitolea mifano Mimi ya namna ninavyocontrol hali hii;

Achana na tabia ya kuspy simu ya Mpenzi wako - Ukipekua lazima utapata sababu ya ugomvi (unless mnaishi kwa kuigiza).

Muamini Mpenzi wako nawe jiamini - Msipoaminiana mtagombana hata bila sababu.

Iko hivi, ukiona mtu kakusaliti na akafanya ujue basi funga vyako anza upya maana hakuna mapenzi hapo.

Kikubwa achaneni na simu za wapenzi wenu.
 
Mi kuacha ku spy simu ya girl wangu labda ni we mfu,maana ishanisaidia sana kujua ukweli.Yani unamaanisha uko tayari kuibiwa ila tu usijue?
 
...ila ukianza kuspy tu...baasi huachi inakua addiction...siku zote unakua mtu wa waswas mnooo juuu ya mpenz wako...na hio ni mbaya zaidi...siku zote uaminifu ni priority namba moja ktk mahusiano....
 
Tatizo sisi wanaume naamini tulio wengi tunapenda kuspy simu za wanawake wetu lakini simu zetu hatutaki tuulizwe maswali wala kuguswa..
 
Tatizo sisi wanaume naamini tulio wengi tunapenda kuspy simu za wanawake wetu lakini simu zetu hatutaki tuulizwe maswali wala kuguswa..

sio wote,,,, kujipa presha ya nini..............kama mwizi ni mwizi tuuu.....utabadilisha hadi lini??? jiamini tu...
 
Wengi tunaukubaliushauri wako na tunaufaham lakini kuufanyia kazi ndio kazi
 
Ni upimbi kumchunguza manzi ako na ikiwa unajua huna uwezo wa kuachana nae.
 
Back
Top Bottom