Hapa nilitarajia ungeielezea japo kidogo hiyo principle kisha ndio tuanze kujadili. Sidhani kama kila mtu anaelewa unaongelea kitu gani. Next time ukiwa unaanzisha mada, nakushauri uzingatie hilo.
Kwa ufupi, Principle of Casuality ni Kanuni inayoelezea uhusiano uliopo kati ya SABABU na MATOKEO (Cause and Effect). Hii ni miongoni mwa nadharia zinazotumika kuelezea mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.
Kanuni hii inaaminisha kwamba kila jambo lina sababu yake. Kwamba, kila matokeo ya jambo fulani, nyuma yake yana kisababishi. Yaani hakuna jambo linalolotokea hivi hivi tu. Na kimsingi ni kanuni inayofuatwa sana kwenye imani za Ubudha (kupitia Karma), kwenye kupata takwimu na hata huko kwenye taaluma ya Uhandisi wa kudhibiti ubora wa vitu.
Kwa watu wa dini, kanuni hii ndiyo imeleta nadharia ya uumbaji. Kwamba hapo Mwanzo dunia iliumbwaje, binadamu alitokea wapi, mwanamke alitokea wapi, shetani alitokea wapi, dhambi zilianzia wapi na kadhalika.
Nadhani nimesaidia kwa kiasi fulani kujenga msingi wa thread yako mkuu wangu
Zurri