PRINCIPAL PASS VYUO VIKUU 2019/2020

PRINCIPAL PASS VYUO VIKUU 2019/2020

karare

Member
Joined
Jun 4, 2019
Posts
31
Reaction score
8
samahani
kwa anayejua principal pass kwa mwaka huu (2019/2020) zinahesabiwaje na inaanzia ngapi mpaka ngapi naomba anijuze.
A=?, B=?, C=?, D=? na kuendelea
natanguliza shukrani
 
A=5
B=4
C=3
D=2
E=1
minimum point kwenda University ni 4, yaani jumlisha masomo mawili uliyofaulu vizuri zikija angalau point 4, basi wewe waweza jiunga na chuo kikuu chochote cha Tanzania kuchukua degree yako. Mfano ukiwa na C pamoja na E tayari point au waweza kuwa na DDF na ukaenda kuchukua degree yako safi kabisa
 
Kwa kujiridhisha soma TCU Admission Guide ya Mwaka huu. Matokeo ya Advanced yanatolewa kwa Grades na NECTA: A=1, B=2, C=3,D=4,E=5, F=Failure, S=Subsidiary pass. Vyuo vikuu na TCU winapo yachakata kwa udahili hubadilisha scores na kuwa A=5, B=4, C=3, D=2, E=1 na S=0.5
Ili ufikiriwe kudahiliwa chuo, tunakuwa na makundi makubwa mawili degree za Afya na la pili degree zisizo za afya. Kwa degree zisizo za afya unatakiwa uwe na point angalau nne za TCU kutokana na masomo mawili uliyo faulu (DD, CE, au juu zaidi). Kuwa na hizo point nne zinakuhakikishia kufikiriwa kwenye udahili lakini hakuna uhakika kwamba utapata. Kupata itategemea na ushindani uliopo.
Upande wa afya wanaweka vigezo hadi vya ufaulu wa somo moja moja na kufanya kudahiliwa kuwa kugumu zaidi. Kwa mfano MD wanataka uwe na Physics=>D, Biology na Chemistry zisipungue C.
Hivyo kama unaomba pitia TCU admission guide ndio ufanye maamuzi.
 
asante sana mkuu
mim nina B moja na E tatu. BEEE
Una point 5 kutoka masomo mawili na jumla ya point 6 kwenye masomo 3. Swali ni kuwa unafikiria degree gani na chuo gani. Ukisha "jua" hilo nenda sambamba na TCU Admission guide uone unafit vipi?
 
asante sana mkuu.
nimekuelewa,
ngoja nianze kufuatilia
 
A=5
B=4
C=3
D=2
E=1
minimum point kwenda University ni 4, yaani jumlisha masomo mawili uliyofaulu vizuri zikija angalau point 4, basi wewe waweza jiunga na chuo kikuu chochote cha Tanzania kuchukua degree yako. Mfano ukiwa na C pamoja na E tayari point au waweza kuwa na DDF na ukaenda kuchukua degree yako safi kabisa
Mkuu Kuna mdgo angu yeye ana C E E E Hapo chuo vipi ni kama 3 ya point kumi na 3
 
Vipi kuhusu EED mkuu?
Soma comment ya Masiya
Kwa kujiridhisha soma TCU Admission Guide ya Mwaka huu. Matokeo ya Advanced yanatolewa kwa Grades na NECTA: A=1, B=2, C=3,D=4,E=5, F=Failure, S=Subsidiary pass. Vyuo vikuu na TCU winapo yachakata kwa udahili hubadilisha scores na kuwa A=5, B=4, C=3, D=2, E=1 na S=0.5
Ili ufikiriwe kudahiliwa chuo, tunakuwa na makundi makubwa mawili degree za Afya na la pili degree zisizo za afya. Kwa degree zisizo za afya unatakiwa uwe na point angalau nne za TCU kutokana na masomo mawili uliyo faulu (DD, CE, au juu zaidi). Kuwa na hizo point nne zinakuhakikishia kufikiriwa kwenye udahili lakini hakuna uhakika kwamba utapata. Kupata itategemea na ushindani uliopo.
Upande wa afya wanaweka vigezo hadi vya ufaulu wa somo moja moja na kufanya kudahiliwa kuwa kugumu zaidi. Kwa mfano MD wanataka uwe na Physics=>D, Biology na Chemistry zisipungue C.
Hivyo kama unaomba pitia TCU admission guide ndio ufanye maamuzi.
 
HUPATI MKUU, LAZIMA UWE NA DB. iyo E imekuharibia
Mimi mwaka Jana nimeingia chuo na MTU ana EEC na anachukua degree, kuna jamaa alikuja kuchukua diploma akiwa na EEC kufika tukamwambia kwa nini hakuomba degree akasema hana vigezo tukamwambia unavyo mwisho wa siku mzazi wake alikuja chuo kufanya mpango achukue degree wakamwambia kaishachelewa ikabidi jamaa akatishe masomo kusudi mwaka huu unakuja kuanza ndio aombe upya kama degree. Acheni kupitosha umma S pekee ndio sio principle pass yakawamba ukapata SA ukategemea kwend chuo ila ukipata E na ukafikisha point 4 basi degree inakuhusu
 
HUPATI MKUU, LAZIMA UWE NA DB. iyo E imekuharibia
uthibitisho huo hapo
Screenshot_20190713-162841.jpeg
 
Tambua kwamba km unadaraja la 3 no chuo kikuu
Kimsingi hawaangalii daraja bali ufaulu wako. Je unamasomo uliofaulu ambayo yana point 4 au zaidi za TCU? Wengi wenye ufaulu wa daraja la 3 point za mwanzo wanakuwa na vigezo vya kuomba. Kuchaguliwa ndio inategemea ushindani hivyo ukichagua chuo na program (course) vizuri una nafasi kubwa ya kupata.
 
Back
Top Bottom