Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,664
This is deep and very relatable. Mimi nilienda kupiga boksi nikiwa bado teenager. Kwa hiyo kimsingi nimeanza kuishi peke yangu mbali na wazazi wangu nikiwa na umri mdogo sana.
Kwa watu ambao hawanijui, wanaweza kudhani labda nimekulia kwenye mazingira fulani ya kudekezwa hivi. La hasha! Maisha ya Marekani kama huna skills za maisha ni magumu sana hususan ukiwa bado mdogo.
Nisingekuwa na nidhamu, hekima, busara, na common sense basi leo hii ningekuwa nimeshafulia kabisa na huenda hata ningekuwa jela au marehemu.
Lakini nashukuru kubahatika kurithi sifa bainishi ya common sense kutoka kwa mmoja wa wazazi wangu (nadhani kama siyo mama mzazi basi atakuwa babu mzaa mama).
Peer pressure ni kitu kibaya sana. Nimeona jamaa wengi sana waliokuwa wanabeba boksi waliopotoshwa na hizo pressure na sasa maisha yao hayana mbele wala nyuma.
Hii observation nayo iko on point sana hususan hiyo namba mbili. Kwa watu analytical na observant kama mimi, hii sifa ni baraka na laana.
Binafsi huwa nachanganua hadi cadence ya mtu. Na kwenye observation huwa naenda mbali mno hadi najistukia mwenyewe.
Hivi kwa mfano tu, ni nani humu huwa anajaribu kuangalia kama mwanamke ana nose hair zilizochomoza? Na kama anazo kwangu ni kama deal breaker flani hivi.
Kwa hiyo nakuelewa kabisa unaposema wakati mwingine ukitumia akili (na ukiwa na akili sana) kwenye mapenzi si vizuri kabisa. Kila utayekutana naye utamwona ana kasoro tu na labda hakidhi vigezo vyako na blahze blahze kama hizo.
Kuna jamaa zangu wengi wanaishi Boston, sijui ndio nyie!
Mama nyumba kubwa heshima kwako..na hii ndo dilema tunayopata maana..kusema ukweli african american woman hawaoleki-wachache sana wenye attitude nzuri..na kuvuta mtu kutoka bongo huwezijua anaweza kuja kukujimbia tumeona haya(hasa wale mademu mawenge wenge na walimbukeni).. Ni kazi sana..na usr bachelor ndo unazidi kukolea..dahUsivute mke toka Tz ...utajutra...labda utafute waliokuja US kusoma...jichanganye utapata mke...lakini usitumie mtu nauli...narudia utajutra na hao ma opportunist....
Wadau kama utamaduni wetu
wa Kitanzania nimewekewa pressure ya juu sana ya kuoa!. Umri wa miaka 38
kwenda 39 sasa pressure imekuwa juu sana kama unavyojua utamaduni wetu.
Mimi nilivyokuja US kama vijana wengi ambao tulimaliza shule miaka ya
kati ya 1990s tulikuwa hatujui vizuri tunakuja huku kwenye nchi
nyingine na mazingira yatakuwaje. Hivyo vijana wengi tumeanza kuwa
wenyewe bina watu wazima wa kutuangalia au kutupa mawazo kuanzia miaka
21!. Pamoja na kuwa na uhuru wa hali ya juu hasa hapa USA vilevile
tumekuja kwenye utamaduni wa kujitegemea sana. Mapema sana kwenye safari
yetu ya maisha ya hapa ilibidi tuchague maisha gani tunataka kuna
waliochagua kujirusha, kupiga deals na kujichanganya na wengine tuliamua
kujaribu kujisomesha na kutafuta kazi au biashara huko mbele. Kwa
tuliochangua kwenda shule na kukimbia matamani ya hapa USA tulijaribu
kupunguza au kuacha vitu Fulani vinavyo punguza mwelekeo wa maendeleo.
Pamoja na vitu ambavyo mimi binafsi niliamua kupungua ni wanawake/kukaa
nawanawake na kuacha pombe. Hii ni baada ya kuona matatizo vijana
wenzangu waliyokuwa wanapata. Nilisema nitaacha vishawishi mpaka nipate
green card na kumaliza elimu ya degree. Mungu akanibariki lakini tatizo
ni moja tu elimu ya kujisomesha hapa USA sio rahisi na degree ya kwanza
hapa ni ndefu sana hivyo nilisubiri green card yangu kwa miaka mitatu
ili niweze kulipia shule kwa bei nafuu kwama wenyeji. Kupiga mahesabu na
elimu ya kusua sua nilimaliza chuo nikiwa na miaka 31 kitu ambacho ni
cha kawaida kwa watu wa kuja kama mimi. Nilifanikiwa kupata green card,
kazi nzuri na kila kitu ambacho nilikuwa nataka. Tatizo ni kwamba baada
ya kuweka ule utaratibu wa kujiheshimu na kupunguza vishawishi sasa
umekuwa kama utamaduni siwezi kurudi kama zamani. Pamoja na kwamba hii
tabia imenisaida kimaisha kwenye kazi na pesa haijanisaidia kwenye
maisha ya familia. Watu naokutana nao kwenye kazi si wabongo na hata si
waafrica, sehemu nayoishi haina watanzania wengi au waafrica wengi sio
mji lakini sihemu ya makazi/mtaa. Umri wa kwenda madisko na kujirusha
umepita na napenda kukaa nyumbani na kufanya mazoezi. Kwa ufupi maisha
yangu naweza kuishi mwenyewe bila wasiwasi. Tatizo lingine ni kwamba
unavyozidi kuwa mtu mzima vitu viwili vinajitokeza kuhusu mahusiano (1)
Unakutana na wanawake wengi wenye matatizo sana kwenye background zao
(2) Unakuwa na akili sana ya kiutu uzima na unajua weakness haraka sana
za watu. Kuwa smart sana kwenye mapenzi wakati mwingine sio nzuri.
Napenda kuwa na familia lakini sitaki kuwa tu na mtu yeyote kwa sababu
ya kuwa na familia.
Sasa na pressure kubwa sana wazazi wangu hatuwezi kuongea kitu kingine
ni kuoa tu! Cha ajabu nafanyiwa connection za watu ambao siwajui kabisa
na marafiki wengine wananipa namba na picha wa wanawake tofauti ambao
sijawahi kuwaona eti niwapigie simu. Pamoja na nia njema za hawa ndugu
na marafiki nafikiri tatizo langu kubwa ni mazingira. Naogopa kuongea
hawa madada kwenye simu na wenyewe kufikiria wanaenda kuolea na jamaa
marekani wakati hata hatujuani. Pamoja na kwamba sijauliza waunganishi
wengi wamekuwa wakinipa viwango vya elimu vya hao madada na picha za
vishawishi na kuonyesha uzuri wao. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha
yangu najihisi kama nilifanya makosa kwa kuwa kama nilitokomeza kabisa
mahusiano yeyote ambayo yangeweza kunirudisha nyumba kwenye nia yangu ya
elimu na kazi pamoja na mafanikio. Sijajua bado nitafanya nini lakini
nitafanya maamuzi yangu mwenyewe kwani mwishoni mimi ndiye nitakuwa na
familia na sio mtu mwingine. Naotoa somo tu hasa kwa wale wadogo
zangu
Kuchelewa kumaliza chuo/elimu ya juu sio tatizo sana coz kwa wengi wetu finances zilikuwa magumashi kwa hiyo ilibidi tuchelewe kidogo. Tatizo kwa mleta mada ni kutojichanganya na wadada hasa alipokuwa late twenties and early thirties. Kujichanganya ni muhimu sana pia huwa akili ya mapenzi ni tofauti na akili ya kawaida. Ukitaka upime vitu in details kwa mdada huwezi kupata mtu wa kuoa...coz hayupo mtu perfect.
Umri unapozidi kwenda choice inazidi kupungua ...si kwa wanawake wala wanaume...possibility ya kupata magumashi ni kubwa sana ...kwa sababu huna muda tena wa kuchunguza...mfano wengi tuliolewa na watu ambo hatukuanza kujuana kwa gia ya ndoa...ndoa ilikuwa matokeo ya kiridhika kuwa tunaendana na tunaweza ishi pamoja.. .
Lakini umri ukienda kila relationship inakuwa serious hata kama hai deserve...
kwa kuwa unakimbia na muda...
it seems wewe ni domo zege maana kwa maelezo yako unasuuzia ulikuwa unatafuta maisha as if ulihama dunia kwenda sayari ya MARS kutoishi na watu usiowajua si sababu ya kutokuwa na mtu kwa umri wako.. huwa huna socialization activities hapi ulipo kwenye nyumba za ibada, kutembelea marafiki etc. BADILIKA kiongozi maisha si kazi/pesa tu
Wewe huna tofauti na Dr. Lwaitama yaani yeye kitabu mwanzo mwisho mambo ya nyuchi hana hata kwenda kusali anaona kama anapoteza muda zaidi hata kununua gari anajionea shida imefika wakati anahoji kwa nini watu tunavaa nguo na wakati mababu zetu walikuwa wanatembea uchi. Huko Marekani kwa jinsi ulivyo eleza stori yako nina wasi wasi utakuja kuolewa na wanaume wenzio maana ndo zenu
Hivi why do indian arranged marriages have a higher success rate then most other marriages hata kwa walioko western world?