Presidential appointees - nani wa kulaumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Presidential appointees - nani wa kulaumiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kidudu Mtu, Dec 11, 2009.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kisa cha DC na DED kutoelewana kwa miezi kadhaa bila ya hatua kuchukuliwa kuweka mambo sawa.

  Nadhani tatizo ni kuwa wote huteuliwa na Rais na hivyo ndiye mwenye mamlaka ya kuwachukulia hatua na hata kutengua uteuzi wao. Hii inaonyesha jinsi mlundikano wa madaraka kwa mtu mmoja (Rais) unavyoweza kuathiri utendaji kazi hasa pale maamuzi ya haraka yanapotakiwa.


  Serikali yawa bubu msuguano wa DC na Mkurugenzi Bagamoyo

  Serikali imekataa kuelezea uamuzi wake kuhusu uhusiano mbaya uliopo kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Rhoda Nsemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Magessa Mulongo, ambao unadaiwa kusababisha shughuli za maendeleo ya wananchi wilayani humo kuzorota.

  Hatua hiyo imedhihirika, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani, kukataa kuelezea uamuzi wake kuhusu tatizo hilo licha ya Mkurugenzi Mtendaji huyo kuiomba serikali kuu kuingilia kati tatizo hilo ili kurejesha maelewano na maendeleo wilayani humo.

  Kombani alikataa kutoa msimamo wa serikali alipoulizwa na Nipashe wiki hii kueleza uamuzi wa serikali kuhusu uhusiano huo kati ya Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu huyo wa Wilaya.

  “Wasiliana na mkuu wa mkoa, tunaenda kwa protocal (itifaki),” alisema Kombani kwa ufupi.

  Alipoelezwa na Nipashe kuwa Mkurugenzi Mtendaji ameiomba serikali kuu kuingilia kati tatizo hilo, Kombani alishikilia msimamo wake wa kutaka suala hilo aulizwe mkuu wa mkoa kwa kusema: “Mkuu wa Mkoa ndiye serikali kuu ya mkoa na mkuu wa wilaya ndiye serikali kuu ya wilaya. Hiyo ndiyo itifaki ya serikali.”

  Nipashe iliwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Hajati Amina, ambaye naye alikataa kuelezea uamuzi wa serikali kuhusu tatizo hilo, badala yake alimtaka mwandishi awasiliane na uongozi wa wilaya, au wananchi au viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo. “Sina cha kuzungumza. Serikali kuu iko pia wilayani,” alisema Hajati Amina.

  Alipoelezwa kuwa kwenye uongozi wa wilaya ndiko uhusiano mbaya uliko kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Hajati Amina alisema: “waulizeni wananchi, pia chama kipo. Mimi sijui kama kuna ugomvi, naomba nisizungumze kitu ambacho sikijui”.

  Wiki mbili zilizopita, Mkurugenzi Mtendaji huyo, alizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), wilayani humo na kuiomba serikali iingilie tatizo hilo, kwa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mmoja wao au kumhamisha kikazi, kwa vile hali hiyo imekuwa ikisababisha shughuli za maendeleo ya wananchi kuzorota.

  “Mimi na Mheshimiwa DC (Mkuu wa Wilaya) hatupikiki kabisa, kuna tatizo kubwa kati yetu. Naiomba serikali kuu iingilie kati, ama ichukue hatua za kinidhamu au uhamisho. Mimi ni Mkristo nabeba msalaba, siridhishwi kabisa na hali hii kwani maendeleo ya wananchi yanakuwa hayapatikani,” alisema Nsemwa.

  Alisema uhusiano mbaya kati yake na Mkuu wa Wilaya umekwenda mbali zaidi kwani tangu Agosti, mwaka huu, wamekuwa wakinuniana na kwamba, wamekuwa wakiongea kupitia Katibu Tawala Mkoa (RAS).

  Alisema hali hiyo imekuwa ikimkosesha amani kiasi cha kufikia kukata shauri la kutaka kuandika barua kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuomba kujiuzulu kazi ndani ya saa 24, lakini amekuwa akizuiwa kufanya hivyo na baadhi ya jamaa zake wa karibu.

  Alipoulizwa sababu gani iliyowafikisha yeye na Mulongo katika hali hiyo, Nsemwa alisema hajui sababu ni nini, lakini ana wasiwasi huenda inatokana na Mkuu huyo wa Wilaya kufanya kazi bila kujua miongozo ya serikali.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mulongo alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na madai yaliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji huyo, hakuwa tayari badala yake akasema: "(Mkurugenzi Mtendaji) aliamua kuwatania tu... Karibu.”

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndiyo faida ya kuto-encourage system ambayo ni competitive. Vyeo vyaenda kwa kugawiana, kama peremende badala ya kutafuta most qualified personnel. Simply pathetic.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wenzetu wanyamwezi mpaka District Attorney na judges wa mahakama za wilaya wanapigiwa kura.
   
 4. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Salome Sijaona Balozi mpya Japani


  [​IMG]Kikwete picks envoys to Japan, Saudi Arabia and Burundi
  PRESIDENT Jakaya Kikwete has appointed new ambassadors to Japan, Saudi Arabia and Burundi to fill vacant posts. The appointments take immediate effect.
  A statement issued today by the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation said that Ms Salome Sijaona (pictured above) has been appointed Ambassador to Japan to replace Ambassador Elly Mtango who has retired.
  Ms Sijaona formerly served as the Permanent Secretary in the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development.
  The statement said that the president has appointed Prof Abdillah Omari as Tanzania ambassador to Saudi Arabia, to replace retired Judge Khamis Msumi who has retired. Before the appointment, Prof Omari served as the Director of Centre of International Relations in Dar es Salaam.
  President Kikwete has also appointed Dr James Nzagi to be Tanzania’s Ambassador to Burundi, replacing retired Brigadier General Francis Mndolwa who has retired. Before his appointment, Dr Nzagi served as a director in the President’s Office.
  Source:
  Daily News
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Watu hutumia vibaya hiyo Presidential appointement. Ni vizuri Rais aka -appoint political posts kama hizo za wakuu wa Wilaya , Mkoa n.k Mkurugenzi wa Halmashauri na Mashirika ya Umma chief Executives wanatakiwa waajiriwe kwa mikataba . Posts zitangazwe , waombe wafanyiwe usajili na waajiriwe kwa mkataba wa miaka 3.

  Yako Mashirika ya kifisadi ambayo viongozi wake wameteuliwa , tena teuzi za kinyemela , za kuchomekea. Hawa ndio wanauwa hayo mashirika maana hwana uwezo. TZ ZAIDI UIJUAVYO!!!!!!!!!!
   
 6. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - wakulaumiwa ni sisi wananchi tuliomchagua Rais anayewachagua hao appointees wake, au?

  Es!
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako.

  Tuko pamoja mkuu.
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Mazee, unajua hata mimi nilikuwa najua kuwa post za DEDs siku hizi zinatangazwa na watu wana-apply na kuwa interviewed. Sidhani kama bado wanateuliwa. Hivi kuna ubaya gani hata hizi nafasi za uwaziri, ukuu wa mkoa, U-DC watu wasiwe wanakuwa interviewed na chombo fulani angalau kupima uwezo wao wa kiutendaji ili kuepuka mambo ya hovyo kama haya ya bagamoyo? Haya mambo ya kiongozi akiamka asubuhi anatangaza nimemteua Mr. XX kuwa waziri, naibu waziri, RC au DC bila ya kuwepo utaratibu wa kuwa-screen ni hovyo kabisa..
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Watanzania sasa tujuilize on a serious note, nchi ni maskini, maendeleo bado hayajaonyesha surge ya kwenda mbele; JE TUNAHITAJI DC NA DED KATIKA WILAYA ZETU? KWANINI MMOJA ASIFANYE KAZI ZOTE???
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  we have very huge administrative structures with very little to manage and very low output if not zero output... worse enough, despite huge admin structures, our accountability is very low
   
 11. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii nimeipenda sana! Hili ndiyo tatizo letu. Wala hawana job description ya kueleweka hawa! Na siyo hapo tu, Kuna Wizara kibao hazihitaji Naibu Waziri lakini wapo kibao! Inakuwa kama wanakua pale kama "standby Ministers". Wizara ina Waziri ina Katibu Mkuu sasa Naibu Waziri wa kazi gani??? Kwanza kuna Wizara zinatakiwa kuunganishwa. Nchi Maskini kama yetu haihitaji Mawaziri wengi kiasi hiki. Huko ni kurudisha shukrani za uchanguzi, ni kugawiana keki ya nchi kinyemela.
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,931
  Trophy Points: 280
  Mkuu wewe huzungushi maneno, safi sana. Nafikiri umefika wakati wa sisi wenyewe wananchi kukaa mbele ya vioo na kujiporomoshea matusi,kebehi na lawama zote kwa maamuzi yetu mabovu tuliyoyafanya na inavyoonyesha tutaendelea kuyafanya.
  TUNAPANDA BANGI TUKITEGEMEA KUVUNA MCHICHA? LOH!
   
 13. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #13
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kusahihisha...wakurugenzi wa halmashauri huteuliwa na Waziri Mkuu chini ya dhamana yake ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Hawateuliwi na Rais.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huyu wanamficha huko kwani anajua siri za ufisadi pale ardhi
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Ugomvi wa DED na DC wa Bagamoyo....nasikia DC analazimisha mafungu toka halmashauri...kwa ajili yake na ofisi yake...safari zake zote na posho analamisha apewe toka kwa DED ukute pia anadai toka office yake...takukuru mpo???fuatilieni suala hili kule watu watarushiana makonde DC labda anamuonea sababu ni mwanamama....
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Hapana!!
  Lawama zielekezwe kwenye Katiba ya nchi iliyoweka taratibu zinayoruhusu watu wadhaifu na hata wazembe kuweza kushika wadhifa wa Rais, ikashindwa pia kuweka misingi rahisi ya kumushikisha adabu kiongozi mzembe.
   
Loading...