Fikra za kinguruwe hazitatufikisha pema peponi.Yeye hajalazimisha media wala public kumsikiliza au kumzungumza. Kama tunavyoamini sote kuwa wapo wanaomzungumza kwa ubaya vivyo hivyo inatupasa kuamini kuwa wapo wanaomzungumza kwa mazuri.
Lakini mbona tunakosa hekima,Ukimwi ni siasa jamani? Nani kasema ukimwi unaua wasio mafisadi tu?? Lakini pia iweje muone ninyi JF au wanahabari tu ndio mnaotueleza ukweli na kujipa wasifu wa kuhukumu wengine,kwani Ben anagombea cheo gani hapa nchini kwa sasa? Sidhani kuwa Ngoma ndio impatie umaarufu,he is already famous,hahitaji makofi wala mchanga.
Msiwachanganye wabongo kwa agenda zenu za kufunika kombe mwanaharamu apite,nchi iko tete inahitaji jitihada za dhati itengamae ,sasa baadala ya kumsaidia muungwana kwa udhati mnajifanya kumpekecha Ben kwa ,hoja za kipuuzi,sasa mkipewa ANBEN,Kiwira n.k ndio Tanzania itagomboka??? Umaskini wetu haukuja kwa dharura,kukosa ujasiri ktk nia ya kuwa wajasiriamali,south africa ni ushahidi wa uzuzu wetu,sasa amekuja mwanaume kuonyesha njia ,imekuwa taabu kila mwana JF,Chadema,CCM-chipolopolo oooh mwizi mwizi,na sisi sasa tutangaze kuwa stori yenu dhidi Ben inapauka,tafuteni mwingine.
Tusiwe wavivu wa kufikiri na kuadhimia mbele kama kweli tunataka maendeleo.