Prado latumbukia Daraja la Tanzanite

Kama wanaongea wangetaja majina yao tukaenda kuwapa pole yawezekana ni ndugu zetu. Kitendo cha kutowataja majina kimeacha walakini. Unaweza ukute ni vigogo wawili kila mmoja na pisi lake.
 
Kwa hiyo askari wa zimamoto na uokoaji wamefika eneo la tukio wakakuta majeruhi washapelekwa hospital? Kwamba taarifa walichelewa kuipata ama?
 
wameshatuharibia daraja la garama kabisa, kuweni makini kuendesha hayo magari. halafu maprado ya aina hii sijui yamerogerezewa ajali?l hii miprado ya zamani.
 
Mambo ya tungi za wikiendi
Siyo kweli mzee wangu, tungi hatukutumia kabisa. Tulikunywa tu bapa kubwa sita sita kila mtu tukaondoka zetu.

Tulipofika darajani na kwa kuona yale mataa na zile grill pembeni ya daraja tukajua tumeshafika nyumbani.

Dereva kapiga honi weee lakini mlinzi hakufungua geti. Kuona muda unaenda na mlinzi haji kufungua, tukamwambia dereva: Ingia na geti ndani.

Mara puuuu dereva kagonga mgeti ule, ila tulipoangalia nyumba yetu hatukuiona. Gari nalo likaanza kuelea kwenye maji kama vile boti la kilimanjao VI ya Azam marine.

Ninachokumbuka cha mwisho ni kusikia watu wakipiga kelele: wanazama hao, wanazama hao lakini baada ya hapo sikimbuki tena lolote.

Ingawa nimeumia lakini bado naziwaza baba zangu nne zilizokuwa kwenye gari. Sijui nitazikuta?
 
So le
Okk Let's put like this "Everyone is innocent until proved guilty " ...
 
Most likely. Prado ni gari ya kishamba sana. Lkn ndio gari inayoongoza kununuliwa na washamba waliookota viela na magari hawajui
nilishawahi kusafiri toka mwanza hadi dsm kwa liprado kama hilo. roho ilikuwa mkononi. mengi yakitoka dsm au mwanza yakipita singida bila ajali shukuru Mungu. nashangaa kwamba hata ndani ya mji kama dsm yanazingua. sasa, hilo daraja nani atagarimia kulitengeneza sasa? tujadili hilo pia.
 
Na Prado siyo gari stable barabaran
Mwezi uliopita uliua ndugu wa4 pale chalinze,watu wasahaulifu sana
Gari unaisingizia.Huwezi kupima ustable wa gari kwa mwendo kasi kwa hizi barabara zetu.jazia na control ya dereva husika ikoje.Ile ya chalinze inaonekana dereva alimwaga moto akakutana na taa kali machoni gari ikamshinda akahama.Lawama tunaitupia gari.
 
Prado limekunywa maji chumvi halifai tena
halikutakiwa kuharibika ili liuzwe pesa irekebishe hilo daraja tulilogarimia kwa pesa zetu za kodi. nawaombea wapone ila hapo darajani ni eneo ambalo hutakiwi kutembea kilometer zaidi ya 30, na kwa mwendo wa aina hiyo usingetumbukia darajani, lazima aidha alilewa au alikuwa kasi, madhara yake ni kwenye afya zao na kutuletea hasara ya daraja tulilojenga kwa kodi zetu.
 
Naskia mlivokuwa kwenye maji mlikuwa mnapiga mbizi kama mko kwenye swimming pool
 
Sio kweli. Haya magari yana tabia za kuchomoka tairi za mbele na kuacha bara bara.
Gari haliwezi kua na tabia.Hatufanyi service za uhakika alafu tunasingizia magari.Ingekua ni lenyewe tu ndo linapata ajali sawa.Lakini ukisafiri unakutana na ajali za magari ya kila aina.Mimi siamini sana kwenye mapungufu ya gari kama mimi dereva nitakua mwangalifu kuanzia kwenye ubora na mapungufu ya chombo changu,barabara na utimamu wangu mwenyewe.
 
Sio kweli. Haya magari yana tabia za kuchomoka tairi za mbele na kuacha bara bara.
ukitembea kilometa ngapi kwa saa? kwa ninyi mliosoma pale darajani, tunatakiwa kupita kwa km ngapi? si ukute 20km/hr. huo ni mwendo mdogo sana hata tairi likichomoka huwezi tumbukia majini.
 
Senge sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Polisi wanatakiwa wawe wanakaa kumbe zote za starehe kuanza piga fine madereva wote walevi mtu akianza endesha gari ametoka Club polisi wampime kiwango cha pombe
Dah! yaani polisi walivyo wachache waache kulinda raia na mali zao wadili na walevi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…