CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 854
Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya firauni.
Mfuko wa jamii wa PPF ni moja ya mifuko ya ajabu sana duniani, kadhalika Mamlaka inayosimamia mifuko hii ya jamii, SSRA--nayo ni ya ajabu zaidi duniani.
PPF kama mfuko wa jamii, upo chini ya uangalizi na usimamizi wa mamlaka inayojulikana kama SSRA. Hawa SSRA wapo nchini Tanzania na ndiyo pia wanasimamia na kuiangalia mifuko yote kama vile NSSF, LAPF, GEPF, na PPF wenyewe.
Tangu Mei 11, 2016, mfuko wa jamii wa PPF umesitisha utoaji wa mafao kwa wateja wake kwa kile wanachodai, kutekeleza sheria ya mifuko ya jamii na ile ya SSRA; Kwa sababu hiyo, hawatoi mafao kwa wanachama wake mpaka wanachama hao watakapofikisha umri wa kustaafu wa miaka 55 au 60. Lakini wakati PPF wanasitisha utoaji mafao kwa wanachama wake kwa sababu zao, mifuko mingine kama vile LAPF wao wanatoa mafao kwa wanachama wake bila mizengwe yoyote ile. LAPF wanatoa mafao kwa wanachama wake waliopoteza ajira au hata kuacha kazi wenyewe.
Wakati PPF hawa hawa wanadai kusitisha utoaji mafao kwa wanachama ambao hawajafikisha umri wa kustaafu, ni PPF hawa hawa wanaotoa mafao kwa watu waliopunguzwa makazini (redundancy); Lakini wale ambao wamefukuzwa makazini hawapewi mafao yao kwa sababu zilezile za kutekeleza sheria ya mifuko ya jamii na ile ya SSRA kama wanavyodai.
Swali linakuja, ni kwa sababu gani watu waliopoteza ajira kwa kupunguzwa kazini wapewe mafao, ila wale waliofukuzwa kazini wasipewe mafao yao? Je huu kweli ni utekelezaji sheria ya mifuko ya jamii au ni mizengwe na ubababaishaji ndani yake.
SSRA ambao wapo nchini na ambao ni wasimamizi wa hii mifuko ya jamii wanafahamu haya. Kwa nini sasa wanashindwa kuingilia kati hili? Je, kuna nini nyuma ya pazia? Serikali inayojiita ya wanyonge inayafahamu haya kupitia wizara ya kazi na ajira, mbona inashindwa kuwasaidia hawa wanyonge?