Powered by Android.

Powered by Android.

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
21,854
Reaction score
26,094
Asalaam aleykum Jamiyah, hapo awali kidogo ukinnunua simu dukani ilikuwa ni simu ambayo endapo ni Samsung, Nokia, tecno na kadhalika, wakati wa kuiwasha ilikuwa inakuja nembo halisi ya simu husika bila ya kuwa na andishi lolote linaloambatana yaani linakuja neno Samsung na mbwembwe zake kwenye screen kwa raha kabisa, lakini kwa sasa inakuwa tafrani kidogo simu nyingi mara ununuapo huja na maneno "powered by androids" pia nyingi huwa zinapatikana moto kwelikweli ambazo ndizo simu nyingi mno, Je simu hizi sio fake?
#Tujuzane wabobezi.
 
Huo ni miongoni mwa ududu ambao utaukuta android,kitu kinawekwa sehemu isiyotakiwa bila sababu za msingi,mbaya zaidi logo na maandishi husika havina ubunifu kabisa kama kiraka.
 
Android ndio mfumo endeshi wa hizo simu, na hii ni moja ya masharti ya leseni kutoka Google ambao ndio wamiliki wa Android OS, ni kama ilivyo kwa simu za iPhone mfumo wake endeshi ni iOS.
 
Back
Top Bottom