Power crisis: Tough times ahead | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Power crisis: Tough times ahead

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,759
  Trophy Points: 280
  2009-10-13 07:42:00
  Power crisis: Tough times ahead[​IMG]Energy and Minerals deputy minister Adam Malima addresses journalists in Dar es Salaam yesterday after attending a meeting that also involved the Parliamentary Committee on Energy and Minerals and the Tanesco board. Others are Tanesco managing director Idris Rashidi (left) and deputy board chairman Semindu Pawa.No solution in sight as sabotage suggestion angers Tanesco boss

  By Vicent Mnyanyika and Paul Dotto

  Electricity consumers appear headed for tough times ahead, with Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) indicating that only torrential rains could save the country from a prolonged power crisis.

  Grappling with rising electricity shortage, Tanesco now subjects consumers to14-hour power cuts throughout the country, and details tabled before the Parliamentary Committee on Energy and Minerals yesterday painted an even gloomier picture.

  Tanesco managing director Idris Rashidi presented members of the committee with a power generation status report that, among other things, indicated that long rains, which are not guaranteed, were the only sure way of easing the power rationing.

  According to Dr Rashidi, other opportunities to increase power generation to ease the shortage of about 100MW on the national grid were anticipated in November. These include the repair of a 20MW Songas turbine that collapsed last month and operationalising the 45MW Tegeta gas turbine, whose implementation has been delayed for technical reasons.

  Other measures to normalise the situation will remain untenable until 2011 and 2013. They include fresh talks to convince Independent Power Tanzania Limited (IPTL), whose contract to supply 100MW had been suspended, to reopen its line and the fast tracking of the supply of 200MW from the Kiwira coal mine.

  Tanesco hopes that heavy rains will start falling soon and fill the dams at Kihansi and Hale hydroelectric plants, which have capacities of 60MW and 8MW, respectively, and raise the outputs of other hydro stations to fix the situation in the interim.

  The situation has not been helped by reports that investors are apparently shying away from taking up an opportunity to invest in a $70 million (Sh98 billion) emergency power-generating contract. Energy and Minerals minister William Ngeleja has been quoted as saying the planned project had not attracted any bids.

  The committee's briefing meeting was held in Dar es Salaam and attended by top Tanesco officials led by board chairman Semindu Pawa and Energy and Minerals ministry officials led by deputy minister Adam Malima.

  The meeting was held against a backdrop of a growing power supply crisis, with industry watchers fearing a scenario worse that what was experienced in early 2006 when the country went without electricity for up to 24 hours in some places.

  Yesterday, according to sources who attended the meeting, Tanesco bosses put up a spirited defence against allegations of neglect or sabotage, with Dr Rashidi saying an imbalance between demand and generation was to blame for the current rationing.

  He said Tanesco could only produce 697 MW against a demand of 769MW. Decreased generation is blamed on falling water levels at hydro-dams due to drought.

  An MP, who spoke to The Citizen on condition of anonymity because he is not the committee's spokesperson, said a report by the committee chaired by Bumbuli MP William Shelukindo had also absolved Tanesco of blame for the latest power rationing.

  Dr Rashidi later rejected questions from reporters who wanted to establish if Tanesco had a hand in the situation. He was also angered when reminded of his remarks early in the year, when he warned that failure to buy the controversial 100MW Dowans power plant would lead to a power supply deficit around this time.
  But Mr Malima denied the ongoing countrywide power rationing was as a result of sabotage. The deputy minister said the capacity to generate electricity had been greatly reduced.

  Mr Malima was forced to intervene and answer questions from reporters after Dr Rashidi failed to explain his prediction that the country would be plunged into darkness if the Government did not buy the Dowans plant.

  Mr Malima said: "There is no sabotage in the ongoing power rationing, what Dr Rashidi said was forecasting this period as an expert."

  The minister confirmed Tanesco was holding talks with IPTL for the purchase of its power plant should the parties reach a court settlement in a capacity charge payment dispute at the international commercial disputes court.

  Eelier, Mr Shelukindo said his committee had given and approved Tanesco's plans to purchase two generators with a capacity of yielding 160MW for Dar es Salaam (100MW) and Mwanza (60MW).

  Mr Shelukindo also said his committee had directed Tanesco and the Government to make sure their plans do not take long to be completed.

  "The Government told us that they have funds for purchasing these two generators and the process is underway. The committee has welcomed the moves and we are looking forward to seeing implementations," said Mr Shelukindo.

  He, however, warned that the country would remain in limbo should the Government and Tanesco fail to act fast.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,759
  Trophy Points: 280
  Date::10/13/2009Mgawo wa umeme waikoroga nchi
  [​IMG]

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima ambaye amesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Idris Rashid hapaswi kulaumiwa kwa kutabiri mgawo wa umeme.
  *BOSI TANESCO AGEUKA BUBU, WAZIRI AJIBU KWA NIABA

  Sadick Mtulya na Subira Kaswaga
  Mwananchi

  WABUNGE wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini wamesema mgawo wa umeme ulioikumba nchi haujasababishwa na upungufu wa maji kama ilivyoelezwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).

  Aidha, kamati hiyo imeridhishwa na matumizi ya fedha katika mchakato wa ununuzi wa mitambo miwili yenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 100 utakaofungwa Dar es Salaam na wa megawati 60 utakaowekwa Mwanza.

  Hata hivyo, serikali imesema hakuna hujuma yoyote iliyofanywa ila mgawo huo umesababishwa na upungufu wa maji pamoja na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kihansi, Hale na Songas.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Idris Rashid alikataa katu kuzungumzia suala la Dowans akisema kuwa limekwisha kufa.

  "Dowans haipo, Watanzania msahau," alisisitiza," alisisitiza Dk Rashid.

  Kauli hizo kinzani zimetolewa baada ya hivi karibuni wabunge watatu wa kamati ya Nishati na Madini pamoja na Naibu Waziri, Adam Malima kufanya ziara katika vituo vya kuzalisha umeme na kujionea hali halisi.

  "Tuliambiwa kuwa mgawo wa umeme umesababishwa na mambo mawili, kupungua kwa kina cha maji na kuharibika kwa mitambo ya Kihansi, Hale na Songas. Hivyo tukaona ni muhimu kupata maelezo ya uhakika kuhusu mfumo wetu wa umeme." alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shellukindo jana mara baada ya kumalizika kikao baina ya kamati hiyo, serikali na wajumbe wa Tanesco katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

  Aliongeza: "Lakini tumegundua si kweli kwamba kuna upungufu mkubwa wa maji katika Bwawa la Mtera".

  Shellukindo ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli hakuzungumzia suala la kuharibika kwa mitambo hiyo.

  "Lakini tumeridhishwa na mchakato wa matumizi tuliyoiagiza serikali katika Bajeti ya 2009/10 kupitia Wizara ya Nishati na Madini kuipa Tanesco, fedha za kununua mitambo miwili ya kufua umeme wa megawati 60 utakaojengwa Mwanza na megawati 100 utakaojengwa Dar es Salaam," alisema Shellukindo.

  Pamoja na mambo mengine Kamati ya Nishati na Madini iliitaka serikali kuacha kutegemea maji pekee kwa ajili ya kuzalishia umeme.

  "Tumeiagiza serikali kuwa sasa ni muda muafaka ikaangalia njia nyingine kwa ajili ya kupata umeme na si kutegemea maji pekee," alisema Shellukindo.

  Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri Malima alisema serikali iliamua kwenda kukagua mitambo ya kufua umeme ili kujiridhisha na hali ilivyo.

  "Mimi (Malima), kwa niaba ya serikali nikiwa na wataalamu pamoja na Meneja Steven Mabada, tulikwenda katika mtambo wa Kihansi ambao huzalisha megawati 180 kutoka katika mitambo mitatu na kukuta mtambo mmoja wenye uwezo wa kutoa megawati 60 umeharibika," alisema Malima na kuongeza;

  "Na maji yanayoingia katika mto ni madogo na yamekuwa ni madogo zaidi kuliko ilivyokuwa".

  Waziri huyo alisema kwa mfumo uliopo katika Bwawa la Kihansi, maji yanayoingia ndiyo yanayotumika kazalishia umeme.

  Waziri Malima alifafanua kuwa kutokana na upungufu huo wa maji pia kituo hicho kimeshindwa kuzalisha megawati 50.

  Waziri huyo alisema vifaa kwa ajili ya kuutengeneza mtambo huo vipo na wataalamu hao wanatarajia mtambo huo ulioharibika utakamilika Novemba, mwaka huu wakati kina cha maji kitakuwa kimeongezeka.

  "Pamoja na jitihada hizo serikali ina mpango wa kutengeneza bwawa lingine litakalokuwepo kilomita 12 kutoka katika bwawa hili la Kihansi ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 300," alisema waziri huyo.

  Kwa upande wa kituo cha Hale, mtambo mmoja kati ya miwili yenye uwezo wa kutoa jumla ya megawati 20 umekufa na gharama za kuufufua ni kubwa.

  "Ili kufufua mtambo huo ambao ni wa zamani (tangu mwaka 1960) zinahitajika dola za Kimarekani milioni 20," alisema
  Waziri Malima na kufafanua kuwa, mtambo uliobakia ambao ndio mpya kwa sasa unazalisha megawati nane tu kutokana na kuharibika kwa kifaa aina ya valvu.

  "Wataalamu wetu wamesema hadi kufikia Oktoba 16 mwaka huu watakuwa wamemaliza kuukarabati mtambo huo," alisema.

  Kuhusu Mtambo wa Songasi, Waziri Malima alisema mtambo mmoja umekufa hivyo uzimwe.

  "Matatizo katika mtambo huo yalitokea baada ya mitambo kuzimwa na ulipowashwa haukuwaka, wataalamu wakagundua kuharibika kwa 'bearing', lakini baada ya wiki mbili unaweza kurudi katika hali yake ya kawaida," alisema.

  Alisema kutokana na hali hiyo kuna uwezekano wa kupatikana kwa megawati 15 ndani ya wiki mbili hizo.

  Hata hivyo, waziri huyo alisema ifikapo mwishoni mwa Novemba mwaka huu, mtambo wa Tegeta unaozalisha megawati 45 utaingizwa katika gridi ya taifa.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco, Semindu Pawa alisema mahitaji ya umeme kwa nchi nzima ni megawati 769, lakini kwa sasa Tanesco inazalisha megawati 697, hivyo kuwa na upungufu wa megawati 72.

  "Pia kila mwaka inabidi kuwepo na ongezeko la uzalishaji wa megawati 75 linalosababishwa na ongezeko la mahitaji ya wananchi na shughuli za kiuchumi," alisema Pawa.

  Katika hatua nyingine, Malima amemkingia kifua Dk Rashid kwa kumjibia maswali.

  Hali hiyo ilijitokeza jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini na Tanesco, ambapo alitakiwa kuelezea kutoa ufafanuzi wa kauli yake aliyoitoa mwezi Machi mwaka huu aliposema: " … nchi ikiingia gizani Tanesco isilaumiwe".

  Naibu waziri huyo akalijibu akisema: "Dk Rashid alifanya hivyo kama utabiri tu, hivyo hapaswi kulaumiwa kwa lolote kuhusu kauli yake hiyo".

  Malima aliongeza kuwa kauli ya Dk Rashid ilitokana na ushauri alioupata kutoka kwa wataalamu waliofanya tathmini kuhusu hali ya umeme nchini.

  Machi Mwaka huu baada ya mapendekezo ya Tanesco kwenda kwa serikali ya kununua mitambo ya ufuaji umeme ya Dowans kukataliwa, Dk Rashid alionya kuwa Tanesco isilaumiwe kama nchi ikingia gizani.

  Pia Kamati ya Nishati na Madini imesema wiki ijayo itajadili suala la Kiwira. Katika Kikao cha 16 cha Bunge serikali ilitangaza kununua hisa zote za mgodi wa Kiwira ili iumiliki.
   
Loading...