Kiswahili cha Code ni Geresho. Neno hili lilitumika kwenye madodoso ya Sensa ya mwaka 2002 sina uhakika na sense ya 2012 maana sikushiriki katika kuhesabu watu. Ililazimika kutafuta neon la Kiswahili baada ya Mamlaka inayohusika na Sensa ya Watu na Makazi kupata hofu ya kutohoa neno Code kwa kuwa utamkwaji wake unalandana na neon Kodi ambazo hutozwa kwenye bidhaa, kwa wapangaji na kadhalika, hivyo matumizi yake yangesababisha baadhi ya watu kutojitokeza kuhesabiwa kwa kudhania kwamba sense ina mahusiano na kujua walipa kodi waliopo.
Sasa Postal Code linaweza kutafsiriwa kama Geresho la Posta