Posta wanaiba Parcels za wateja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posta wanaiba Parcels za wateja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MVUMBUZI, Apr 30, 2012.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Nataka niamini kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wa posta Tanzania wasio waaminifu na wamekuwa wakipekua na kuiba parcels za wateja haswa zile zinazotoka nje ya nchi. Mimi ni mwaathirika ambaye parcels zangu kadhaa zimepotelea posta licha ya kuwasiliana na wale walionitumia na kusema tayari zimeondoka nchi husika.

  Nasema hivi kwa sababu kuna parcels zenye tracking number na unapotumiwa una track vizuri na mpaka inapoondoka marekani au Asia au UK. Lakini once parcel inapoingia Tanzania unapiga kiguu na njia posta hadi mwezi mzima kufuatilia unaambiwa hatujaiona na hata ukiwaonyesha tracking number watasema hiii number hai track beyond nchi parcel iliko toka na wanakwambia hawana jinsi ya kusaidia. Imenibidi niandike niulize kama kuna watu ambao wamepata tatizo kama langu kwani tayari parcels zangu zisizopungua 5 zimepotea kuanzia 2010 hadi leo. Mwaka huu 2012 umeongoza kwa parcels zangu kupotea nimekuwa nikifuatilia posta bila mafanikio. Licha ya waliotuma kukuhakishia kuwa wametuma parcel lakini tracking number huonyesha mzigo uliondoka nchi husika na kama umepotea ni ndani ya Tanzania.
  Uzoefu wangu unaonyesha parcel zinazopotea ni zile ndogo ndogo za gram kuanzia 200 hadi 400 na zile zilioandikwa "GIFT".
  Hii hali inaongezeka siku hadi siku na Posta isipoangalia imani yetu kwao itapungua kwani hata mimi sina kabisa imani na shirika letu la post haswa kitengo kinachoshughulika na parcels.

  Uzembe mwingine ambao ni meou note kwenye posta ni kupeleka parcels kwenye box number wrong na wenye box kama si mwaminifu kikuta ni kitu kinachomfaa hukichukua.

  Kuna pia uzembe wa ku rekodi majina wrongly ya wenye parcel na kusababisha parcels kupotea.

  Ninahisi hata wale wafanyakazi wanaopokea parcels na ku sort out na kuziweka kwenye Masanduku ya watu wana uwezo mdogo sana na kwa ujumla si makini kutokana na wingi wa parcels. Parcel inaweza ingia sya Arusha jumatatu na inachukua wiki nzima kufikishwa kwenye sanduku la mwenye parcel. Huu ni uzembe unaowapa nafasi wafanyakazi ambao sio waaminifu kuingiwa na tamaa na kuiba vifurushi vya watu.

  Siongei uzushi bali ni ukweli na kama nasema uongo waniambie parcels zangu ziadi ya 5 zilizoingia Tanzania kwa nyakati tofauti zimepotelea wapi?
   
 2. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Mkuu hili tatizo nami nimekuwa nalipata hasa parcel za nje ya nchi na ukienda kufuatilia watakwambia mizigo haijafika .Ukifuatilia zaidi watakwambia imepotelea hukohuko. Hili tatizo limeanza mwaka huu kwani miaka iliyopita mizigo yangu ilikuwa inafika kwa muda muafaka na haikuwa inapotea. Nafikiri posta watathmini wafanyakazi wao waangalie kama ni waaminifu la sivyo itapoteza credibility
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Sasa sehemu gani hakuna wezi Tanzania? Inategemea tu wengine wanaiba bila wewe kujua unaibiwa.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hili tatizo ni la kufuatilia mara moja. Hapo nyuma mambo yalianza kuwa mazuri sasa inawezekana wanarudia madudu yale yale.
   
 5. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kilichobakia kufanyika ni kuibinafsisha sehemu ya huduma za mizigo/vifurushi.
   
 6. T

  Taso JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Vipi alternatives nyingine kama DHL Global ambao hufanya door to door delivery?
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  posta tanzania wanaiba hilo halina ubishi
   
 8. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Pole ndugu. Una hoja na vithibiti vinavyoweza kuwawafunga hao wasiowaamnifu. naomba nikupe ushauri wa bure juu ya parcels zitokazo nje. Hakikisha kwamba zime wekewa bima huko zitokako ili zikipotea bima ikulipe. Nilitonywa na jamaa kwamba wanviogopa vifurushi vilivyowekewa bima na pia waambie wanaokutumia walipie huduma iitwayo delivery confirmation..Hapo utakuwa umewatega pabaya... Lakini jamani wafanyakazi wa shirika la umma/serikali hata binafsi.. uaminifu uwe suala la msingi na kuwa moja ya maadili makuu ya kuajiriwa.
  Kila la heri
   
 9. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yote hayo ya nini wakati DHL ipo? (sitangazii biashara lakini jamaa wapo fit)
  Schenker pia si wabaya ila tu sijui kama huduma zao zipo TZ.
   
 10. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hata DHL wanaiba parcel yangu kutoka USA ilichukua zaidi ya miezi sita na kufika huku nilipewa box tupu nikaambiwa ndivyo walivyo pokea hata wao jamani uchakachuaji kila kona sijui tufanyeje? na wakati mwingine kauli zao sio nzuri sijui nikutokana na kuwa na wateja wenge hawana customer care kwa wateja.

  Asante
   
Loading...