Habari zenu wanajukwaa hili pendwa,
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nikiwa kama mtanzania mzalendo ambaye natumia huduma za posta mara kwa mara kutuma na kupokea mizigo midogo nje ya nchi sasa tatizo linakuja kwa hawa wafanyakazi wa shirika la posta tawi la Kahama ambapo kuna mama mmoja mtu mzima hivi mweupe ana kauli chafu kwa wateja kiasi kwamba unaweza kuuliza kitu ili ueleweshwe ila jibu atakalokupa utajuta!
Mbaya zaidi unapofanya malipo ya huduma au kutuma mzigo ukiomba risiti hupewi huyo mama hupenda kusema kuna shida ya mtandao hivyo risiti hazitoki ukihoji sana anakuwa mkali kiasi kwamba anaweza hata kukutukana.!
Nikiwa kama mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu na maendeleo pia naomba serikali ichunguze huyu mama maana malalamiko ya watu kunyimwa risiti wanapolipia huduma au kuagiza mizigo
Wakati mwingine huyo mama anaweza kukwambia risiti utaijia badae lakini badae ukirudi anakwambia risiti yako imepotea eti wafanyausafi watakuwa wamekusanya na kuitupa!
Mbaya zaidi kauli za mama huyo zimekuwa kero kwa wateja maana amekuwa mkali sana hasa anapodaiwa kutoa risiti.
Najua humu kuna watu kila idara hivyo kama kuna anayeweza kufikisha ujumbe huu kwa wakuu wa idara tafadhali jaribuni kufuatili tuhuma hizi kabla ya kuendelea kupoteza wateja na watumiaji wa huduma za posta.