Post Graduate Diploma v/s Bachelor Degree


Got u well!!
 

nikusahihishe kidogo sio kwamba post graduate diploma anaufaulu mdogo. ila inakupa linki ya kusona masters fulani

mfano ww umesona degree ya law huwezi soma masters nnje ya law hivyo kwa mfano mtu mwenye degree ya law anataka awe na masters ya education bas hapo lazima asome post graduate in education na akimaliza hapo ndo anaruhusiwa kufanya masters ya education

ili kufanya post graduate diploma ni lazima mtu awe na degree.
 

safi sanaaaaaaan big up umeandika nilichotaka kuandika
 
Neno au kiambishi "POST-" maana yake baada ya "after" kwa hiyo,POSTGRADUATE maana ya mafunzo au taaluma anayosomea mtu baada ya kuwa na SHAHADA(1st degree ) mtu ambaye hana shahada au degree hawezi soma kozi ambayo ni post graduate diploma au masters.

Postgraduate diploma ni mafunzo au kozi ya kukupa uelewa au ujuzi fulani juu ya degree yako. Mf, mtu aliyesoma LLB lakini akajiunga na ualimu wa sekondari anarudi masomoni jusomea elimu huyu atasoma POSTGRADUATE DIPLOMA in Education. Au mtu alisoma Bsc Geology lakini hana elimu ya gas and petrofuel anaamua kuongeza ujuzi anawezasoma POSTGRADUATE DIPLOMA in Natural Gas and Petro Fuel.

Swali lako ni je,wa degree na postgraduate diploma wanaweza kuwa na ufanisi sawa? Suala la ufanisi linategemea mhusika pia na elimu na ujuzi katika eneo husika pia na upenzi wake kwenye fani na marupurupu.
 
Kweli wengi tunataka ufafanuzi,ni nani mwenye elimu kubwa kati ya hawa!

postgraduate diploma is greater than degree,although degree holder is more efficient than PGD holder due to time spending on the course
 
Za muda tena wadau wa jukwaa hili!

Naomba kujua je! mtu mwenye post graduate diploma iliyo tofauti na digrii yake ya kwanza anaweza kuwa na ufanisi ulio sawa katika utendaji na mtu mwenye bachelor degree ya kozi husika? Kalibuni sana.

PGD is equivalent to master
 

Asante mkuu!nimekupata vilivyo.
 

Mwenye degree ana akili sana, apa una maanisha nini? Kuwa mwenye diploma hana akili au? Aaahah aahh!! Wewe utakuwa wa division five, umeandika kitoto sana hata sijui kama umemaliza form 4
 

Aaah kumbe na wewe umeliona hili? Nikajua peke yangu, huyu jamaa sio mzima kabisa, hata nashindwa nimuwek kweny group gan, na kama ana degree basi ya kununua, maana hata hao wenye diploma hawana akili mbovu kama zake, aibu sana hii
 
Yaani wewe ndo umehit target...
Kuna watu wamejifanya kujuwa lakini wameishia kutuonyesha ni kwa kiasi gani nao hawajui kama tulivyokuwa wengine.
 
Watu wengi wanafikiri PGD ni daraja tu la kusoma masters kwa waliofanya vibaya undergraduate kumbe pia ni sehemu ya kuongeza ujuzi kwa Graduates ......
 
Post Graduate Diploma inasomwa katika condition zifuatazo

(1) Mtu mwenye PASS na anataka kusoma Master, baadhi ya vyuo vinataka mtu apitie PGD ili wamkubali asome Master

(2) Watu wenye Advance Diploma, Baadhi ya vyuo havipokei watu wenye Advance Diploma kusoma Master mpaka asome PGD ili akubalike

(3) Kwa mtu mwenye degree ya fani fulani kama Engineer, law nk anataka asome fani nyingine ili aongeze ujuzi tofauti au hapo baadaye asome master ya kitu alichosemea kwenye PGD
 
Mambo mawili:
1. Inawezekana wakati wa Bachelor degree GPA za muhusika zilikuwa hafifu hivyo kuwa vigumu kujiunga na Masters Degree. Wakati mwingine mtu mwenye Bachelor anaweza kwa ridhaa tu akachukua PGD tofauti na Course ya awali ya Bachelor Degree ili tu kujiongezea wigo wa uelewa wa taaluma tofauti.

2. Watu wote wenye Advanced Diploma, iliwapasa ili wafanye Masters Degree, lazima wachukue PGD. Zamani vyuo vingi vilikuwa vinatoa Advanced Diploma badala ya Degree: Ardhi University- UCLAS, DIT- Dar Tech, CBE, IFM, TIA- DSA, MUST- MIST- Mbeya Tech nk
 

Yap kaka/mkuu. Uko sahihi kabisa. Nikupe LIKE ya maandishi.

Tuhitimishe kwa kusema tu kuwa PGD ni kubwa kuliko Bachelor Degree na ndogo kuliko Masters Degree!

Pia kwangu mimi, simsemei mwingine kwamba: Advanced Diploma ni Kubwa sana kuliko Diploma lakini ni ndogo( kidogo kwa content) kuliko Bachelor Degree
 

Nakumbuka wakati nipo Undergradutae tulikuwa tunasoma na watu wa Advance Diploma baadhi ya kusoma, na wakati nasoma Master tulikuwa pia tunashea baadhi ya course na watu wa PGD, na wengine niliokuwa nasoma nao Master waliunga tokea PGD

Kiuhalisi hakuna tofauti kati ya Advance Diploma na Undergraduate ila ni kama kuwakomoa tu ili wasome PGD, ila Master na PGD hazipo sawa
 

Una uelewa mdogo pia ktk masuala ya grading. Anza kujua neno prefix na affix.pengine itakusaidia kunyumbulisha. Yeyote mwenye degree/ Advanced Diploma anasifa yakusoma Post (graduate), hii inasababu nyingi kuamua kusoma post,ama ni "academic crossing" au. Ni supportive entry ya masters au willingness. Sifa ya kusoma post/ kigezo kikubwa nikwamba lazma uwe na elimu kubwa kuliko Ordinary diploma.
 

Yeah! Ukiangalia kimantik content ya Bachelor na Advanced Diploma ni sawa kwa 98% japo kuna vitu fulani vinaongezeka au kupungua. Hivyo UDSM wakati ule ( wa monopoly) waliweka sharti hilo. Ama kwa wale wenye Bachelor lakini GP ziko dhaifu ni lazima ufanye kwanza PGD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…