Posho za wabunge ni ufisadi pia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho za wabunge ni ufisadi pia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, Jan 26, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wabunge wa upinzani wasaidie kupunguza posho zao ili kunachobakia kisaidie sekta nyingine tusikae tunapiga kelele kwa pesa ambazo hazijalipwa nadhani itakuwa busara tukianza na hizi zinazolipwa haba na haba hujaza kibaba.

  [​IMG]
   
 2. k

  kayumba JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu matumizi mabaya ya rasilimali za umma yamekita mizizi hata ndani ya bunge.

  Si bunge lililopita tu bali mabunge yote tokea mfumo wa vyama vingi uanze na kabla ya hapo. Hoja ya kutetea masilahi yao ndiyo pekee uwaunganisha bila kujali wapinzani na ccm.

  Kwanza walishajinoneshea malipo na bado hata leo wanasema hawalipwi vizuri inavyotakiwa. Bila aibu utasikia wanajilinganisha na wabunge wenzao wa nchi nyingine. Hii tabia ya kujilinganisha na wa nchi nyingine ni ujinga mkubwa kwa sababu kama nyie (wabunge) mnajilinganisha na wabunge wa nchi nyingine katika masilahi yenu mbona hamtulinganishi nasi wananchi katika huduma za msingi tunazopata kutoka serikalin na huduma za msingi wanazopata wananchi wa uko ulaya! This is unfair

  Ebu ajitokeze mbunge yeyote aeleze ni kwanini wanalipwa Tsh. 2500/= kwa lita ya mafuta wakati mafuta siku zote mafuta uuzwa chini ya 2500/=. Kama hiyo ni haki mbona idara za serikali hawapangiwe flat rate kama hiyo. HUU NI UFISADI MKUBWA, na kudhihirisha hilo utaona kwa sasa mafuta yakifika 2500 watasema hela iongezeke manake haitoshi.

  Wabunge tuelezenin kwanini msilipwe kwa gharama halisi namtoe risti za manunuzi? Wa DSM anunuae mafuta kwa 1700/= na Kigoma anunue kwa 2100/=

  Je tumesahau walivyomshambulia Dr. Slaa kwa pamoja pale alipotaka marupurupu ya wabunge yapunguzwe? Huenda ndiyo maana wananchi walionekana kumshabikia sana Dr. Slaa!

  MWISHO;
  Inapokuja kwenye ufisadi watanzania karibia wote nguo iliyokatwa kwenye kitambaa kimoja!

  TAFAKARI!
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kwa maana hiyo vita ufisadi hawezekaniniki bora tujikite kwenye kutoa ushauri kwenye maswala ya mapenzi na mahusiano?
   
 4. c

  chelenje JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuleni maisha tu, hakuna jipya ...wabongo wenyewe waoga kuandamana, kama vipi tupige kama Tunisia!
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  enyi watanganyika amkeni na mtazame hali halisi ya nchi yenu, hivi hamjui kama ubunge na uwaziri ni biashara?hamuoni jinsi wanavyotumia garama kubwa kwenye kampeni? Hao wabunge wote ni mafisadi.
   
 6. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndio maana wabunge wako radhi kuchakachua matokeo kwa ajili ya mamilioni hayo. Ref Makongoro Mahanga wa jimbo la Segerea
   
Loading...