The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,906
- 2,885
Katika hali ya kawaida mtu anapaswa kulipwa ujira kutokana na kazi anayofanya. Ikiwa kuna watu wameajiriwa kufanya kazi moja kwa malipo sawa lazima kutatokea sintofahamu. Ndicho kinachoendelea sasa ndani ya bunge letu tukufu.
Wabunge wa upinzani wamesusa kuhudhuria vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wake kwa chombo hicho,jambo linalowapelekea wabunge wa CCM kubakia peke yao ndani ya bunge na kufanya kazi zote zilizopaswa kufanywa kwa pamoja huku wenzao wapinzani wakizurura na kufanya siasa nje ya bunge na kusubiri mshiko wao mwisho wa mwezi kama kawaida.
Kwa maoni yangu kitendo cha wapinzani kutolewa nje ya bunge wakati wenzao wako ndani hakina athari yoyote kwao kisiasa kwani historia inaonyesha kua wengi wa wabunge waliowahi kuadhibiwa kwa kufukuzwa bungeni ilikua ni namna mojawapo rahisi sana ya kuwajenga kisiasa.