POSA

POSA

McCarthy

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
506
Reaction score
554
Wanajamvi

Mimi nipo hapa kuna mwanamke ninampango wa kumuoa. Sasa ninataka kutoa posa na bahati mbaya sijawahi kuposa wala kuona mtu akipeleka barua ya posa.

Naomba kuuliza je,

1.Ni nani hasa anatakiwa apaleke nlvarua ya posa? Muoaji au ndugu zake?

2. Je, kwenye barua ya posa unasema nini kwa ufupi?

3. Je, barua ya posa lazima iandamane na pesa. Kama hivyo ni angalau Sh. ngapi?

Nawasilisha wadau.
 
Suala la Posa si la kisheria, ni jambo la kitamaduni hivyo kila jamii inautaratibu wake ktk kumuoza binti, ulizia jamii ya huyo mchumba wako wanafanyaje ili uanze mchakato mara moja..!!!
 
Nilisikia barua inatakiwa iandikwe kwa mkono sio zile za kuchapwa na mashine
 
Wanajamvi

Mimi nipo hapa kuna mwanamke ninampango wa kumuoa. Sasa ninataka kutoa posa na bahati mbaya sijawahi kuposa wala kuona mtu akipeleka barua ya posa.

Naomba kuuliza je,

1.Ni nani hasa anatakiwa apaleke nlvarua ya posa? Muoaji au ndugu zake?

2. Je, kwenye barua ya posa unasema nini kwa ufupi?

3. Je, barua ya posa lazima iandamane na pesa. Kama hivyo ni angalau Sh. ngapi?

Nawasilisha wadau.
Tafuta mshenga wa kabila husika atakuelekeza kila kitu.

Mimi barua aliniandikia, then nikacopy kwa mwandiko wangu kwenye karatasi nyingine. Mambo sio magumu ki hivyo, usiogope.

Kuhusu pesa unayoweka kwenye barua inategemea na kabila husika na upendo ulionao kwa huyo binti.

Mimi niliweka kiasi fulani hivi (sio kikubwa), lakini yule mzee akakubali sana. Usiweke buku 20 kama wanavyofanya wazaramo.

Kila la kheri.
 
Andika barua weka laki mbili ndani, mpe kaka au mjomba au rafiki apeleke.
 
Andika barua. Jitambulishe wewe ni Nani na unatoka wapi na dhumunu lako la kumuoa huyo binti. Kisha weka hela kiasi chochote unachoana kina faa.

Note: usiweke hele nyingi unaweza ukapangiwa mahari kubwa. Wakajua unazo
 
Back
Top Bottom