Portal To Another Universe

plan z

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
1,381
1,414
Moja kati ya vitu ambavyo navifuatilia sana ni hizi theory za quantum physics na kujaribu kuzichambua ili kuweza kuzing'amua kama zina ukweli au la.

Sasa basi yako maeneo ambayo ukiyapita tu, tuseme unatoka sehemu A kwenda B na kikawaida muda unaopaswa kutumia labda ni lisaa limoja ila kuna point ukiikatiza tu, unaweza kujikuta eneo ambalo ulipaswa utumie lisaa limoja utajikuta unatumia dakika ishirini tu bila nguvu yeyote kupotea, bila kuongeza speed yeyote.

Yako maeneo ambayo ukienda tu ukakaa kama dakika tano ukaamua ngoja niondoke, kitendo cha wewe kuondoka tu hapo unaweza ukajikuta ulikaa kumbe masaa kumi, mfano saa tatu asubuhi ulijiambia ngoja nikachimbe dawa pale mbele na ukafanya hivyo na imechukua dakika tano tu ila wakati unarudi unashangaa ni saa kumi jioni.

Maeneo haya nitayahifadhi, sitapenda kuyataja sasa kwa sababu zangu binafsi, ila nitatoa sababu nini kinafanya maeneo hayo yawe hivyo yalivyo.

Nadhani wengi humu mmeshawahi kusikia msemo unaosema ulimwengu wa high self. Yaani your high self ndiyo inayokupa mwongozo, na hii pia ntaifafanua kiasi.

Tuseme mafanikio yako yanatakiwa yatoke point A kwenda B, halafu njiani kabla hujafika point B kuna point C kwahiyo ili ufike point B lazima uvuke point C, hapa kama ulikimbia hesabu inabidi utafakari kwa kina ili nisikuache.

Sasa kwenye hiyo point C kuna msitu wenye wanyama wakali na huwezi kuvuka kiurahisi, kwenye point hii C ndo utaona utoboi na mambo hayaendi, ni point ambayo huoni uelekeo.

Kama uko katika point hii, kitu pekee ambacho unatakiwa kufanya ni kuwasiliana na your high self ili ikupe possibilities.

High self ni nini? Kitu gani tena hicho huyu mwandishi anakizungumzia anakiita your high self? Ina maana high self yangu mimi naijuaje, nawasilianaje nayo sasa, kivipi yani?

Usiogope, your high self ni wewe mwenyewe in another dimension, ngoja niweke mfano halisi, watanzania wengi wanacheza draft, japo mimi draft silikubali kivile, mimi nacheza mchezo mgumu zaidi unaitwa Chess, sasa wacheza draft huwa kuna kuwa na watazamaji, sasa wale wachezaji pale ndani unakuta mmoja wako kete zake zimekaa kwenye position nzuri, ni swala la yeye tu kucheza vizuri sehemu flani ili ambane mpinzani wake na kisha amfunge kirahisi.

Sasa cha ajabu mchezaji huyo wa ndani haoni hiyo better movement anayopaswa kucheza, ila watazamaji wote hata yule ambaye hajui kaiona hiyo better movement, lakini cha ajabu pia mchezaji huyo anaweza kucheza pengine kabisa akija kuonyeshwa ndo anasema aisee, nilikuwa sijaiona.

Sasa high self ni wewe binafsi kwanzia 4 dimension na kuendelea, nikipata mda ntakuja kuzichambua hizi dimensions zipo 11 kibinadamu. Sisi tunaishi 3 dimensions, pia sisi tunauongoza ulimwengu wa 2, 1 na 0 dimensions, na tunaongoza na dimensions za juu kuliko sisi.

Hii high self itakuambia, unaona hilo korongo hapo pembeni ya huo msitu ( point C sasa), achana na hiyo njia ya point C, zunguka kwenye hilo korongo utakutana na mto ambao ni point D, kisha uvuke panda na hiyo barabara nyembamba utatokezea kwenye njia kuu itakayokupeleka point B.

Sasa ngoja nikatishe maana sitaweza kuandika vyote, ni vingi sana ila nitakuwa responsible kwenye comments, nitaendelea kufunguka zaidi kwa kadri maswali yatakavyo ulizwa.

Ila nimewahaidi nitataja conditions kwa nini hayo maeneo yapo hivyo, zipo conditions nyingi ila ngoja niwanyime zingine nitaje mbili tu kwanza.

1. Areas with higher gravitational force
2. Areas with higher dimensions.

Sababu kuu kwanini sitaki kufunguka vyote kwa sasa ni kwakuwa nina youtube channel ambayo nataka nichambue hizi mada kwanza huko, nikizifikia hatua nzuri basi huku mimi nitaandika, lengo ni kuepusha wizi wa ideas.

Ila kulingana na maswalo nitayajibu kwa comments na kufunguka kwa kina, ambayo hayataulizwa basi nitabaki nayo hadi nitakapoyatanguliza youtube.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Back
Top Bottom