Porojo za Kawambwa na ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Porojo za Kawambwa na ATCL

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 31, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,584
  Likes Received: 5,765
  Trophy Points: 280
  HATMA ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), itajulikana wiki ijayo wakati Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa atakapotoa taarifa ya utendaji wa shirika hilo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

  Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, Kamati hiyo itakutana na waziri huyo Aprili 8 kujadili suala hilo na siku inayofuata kamati hiyo itajadili taarifa yake ya mwaka.

  ATCL ilijikuta kwenye wakati mgumu mapema mwaka jana ilipopokonywa leseni ya kuruka angani na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) baada ya kugundulika kasoro kwenye fomu za kampuni hiyo ya serikali. ATCL ililazimika kutofanya safari kwa wiki kadhaa kabla ya kurudishiwa leseni hiyo, hali iliyolifanya shirika hilo lipoteze soko lake.


  Hata hivyo, kwa mujibu wa tangazo la jana la TCAA, kampuni hiyo ambayo iko kwenye mchakato wa kufufuliwa upya, imeomba upya leseni ya usafiri wa anga, ikiwa ni pamoja na kuongeza safari za ndege zake pamoja na ndege za kukodi.

  Suala la ATCL na la Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) yalikuwa yajadiliwe katika kikao kilichopita cha kamati hiyo, lakini yalikwama baada ya Dk Kawambwa kushindwa kutokea na kamati kuvieleza vyombo vya habari kuwa masuala hayo yatajadiliwa na Baraza la Mawaziri.


  ATCL, ambayo ilikuwa na ukiritimba wa usafiri wa anga, ilianza kutetereka wakati ilipoingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka 2001.

  Lakini baada ya matatizo mengi ya kiutendaji, mkataba huo ulivunjwa mwaka 2006, huku ATCL ikiwa imeachwa na deni kubwa ambalo liliifanya itetereke kiuchumi hadi ilipopokonywa leseni ya usafiri wa anga kutokana na matatizo ya kiusalama.


  Habari zaidi zinasema Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, kesho itajadili muswada wa watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wataruhusiwa kutoa maoni yao.


  Kamati hiyo pia itakutana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kujadili maoni ya wadau wa elimu kuhusu uwezekano wa kuwarudisha masomoni wanafunzi wanaopata


  KAWAMBWA ACHENI SIASA KWENYE SUALA LINALOHUSU MSLAHI YA TAIFA

  ATCL INAJULIKANA SHIDA ZAKE NA MPAKA KESHO MNAKALIA MATATIZO YA ATCL.....ACHEN KUWAHADAA WABUNGE...
   
 2. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ATCL kwa serikali ni kama kichaa na mwenda wazimu, Serikali inafanya biashara ya kuuza vitumbua ??? nani kakwambia biashara itaendelea hapo ???? sasa ule umebaki mradi wa watu tu hakuna lolote hapo !!!! Anahitajika mwekezaji wa uhakika na wala si mbabaishaji !!!
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo hapo ni Kawambwa....hana uwezo kabisa kwa kutoa maamuzi just kama JK. Mpeni wizara ya Miundombinu Mh. Dr. John Pombe Magufuli muone kazi.....hiyo ATCL itaweza kuendelea in 2 years.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,584
  Likes Received: 5,765
  Trophy Points: 280
  hilo luba la kawambwa!!!!kamradi chao watalaaniwa maisha na atcl
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  niliwai kuzungumza kuhusu uwezo wa serikali kuendesha mashirika ambayo ni technical zaidi ktk operation zake kama atc, reli, tazara, tanesco, general tyre, uda etc serikalini cost za maintenance kwao ni si muhimu ndio mana mashirika yote hayo yanakufa kwani wanapozinduka cost za kufufua mitambo iliyotelekezwa ni kubwa, pili hawana wataalam kwa fani izo hata wenye nazo hawako uko kwani serikalini ajira ni ya kujuana wakati kuna fani haziitaji mambo hayo, kwa iyo tatizo la atc linaanzia mbali na kuriludisha inaitaji mfumo mzima ubadirishwe kuanzia ajira hadi funding priority! nchi yetu tunaweza endesha mashirika yasiyo ya technical operation kama ma benki, bima, tra, newspaper etc
   
Loading...