Wewe ni mtanzania kweli?
Yaani umechelewa kupigwa picha ya X-ray kwa lisaa limoja tu halafu unakuja kulalamika hapa JF!?
Uko seriously kweli au unatania?
Hospitali zipo nyingi sana, ungesepa zako na kumpeleka mahali pengine akatibiwe, halafu ungeleta mrejesho wa utofauti wa huduma hapa JF.
Kuna mambo ya Foleni za wagonjwa, uchache wa watumishi, mida ya kuchelewa kama jioni nk. ambapo huduma kwenye taasisi nyingi za umma hudorora sana. Kwa Tanzania ni jambo la kawaida mno.
Ni hospitali gani hapa Tanzania yenye kutoa huduma kwa jamii kubwa inayoweza kukupa huduma hiyo kwa haraka zaidi ya huo muda?