Wakuu ushindi wa M4C umechangiwa kwa kiasi kikubwa pia na waheshimiwa wafuatao
Kamanda Lema, mlimuona jinsi alivyokuwa jirani na msimamizi wa uchaguzi wakati wa kutangaza matokeo. Inaonyesha Kamanda pamoja na kuambiwa kuwa Washili watamuua, lakini alipiga kazi ya ukweli kumsaidia Nassari bila hata kujali kuwa ana kesi inayoweza kumvua ubunge wiki hii. Big Up Mh. lema
Pia upande wa CCM, namshukuru sana Nape na Wassira kwa kuachangia ushindi wa CHADEMA. Nape alimpinga Sioi tokea mwanzo japo mafisadi walimzidi nguvu.Wassira yeye pamoja na kumpinga Sioi, alikwenda mbali zaidi kwa kwenda kupiga kampeni za matusi na kashfa ili wananchi waione CCM kama chama kisicho na maadili.
Edward Lowasa nae amechangia kuiua CCM at the same time akiisaidia CHADEMA kwa kitendo chake cha kuwahonga wajumbe ili wampitishe Mkwe wake kwenye kura za maoni na akaharibu kabisa pale alipokuja jukwaani kupiga kampeni kwa ajili ya Sioi. Anajua kuwa Watanzania wanajua kuwa yeye ndo aliyeshiriki kuiua CCM kwa ufisadi wake na wenzie, na kitendo cha kwenda kwenye kampeni ni dalili tosha kuwa aliamua kuisaidia M4C bila kujua huku akiiua CCM. Thanx EL