Waswahili wanasema uungwana ni vitendo, mtu au taasisi zinazofanya vizuri kwanini zisipongezwe. Katika pitapita yangu kwenye channel mbalimbali za TV hususan local TV, sitasita kuwapongeza kwa dhati wadau kwa kuandaa Vipindi mahiri vya masomo mbalimbali na kufundisha madogo kwa kutumia Televisheni.
Ni kipindi kirefu sasa nadhani kuanzia mwezi Marchi mwishoni hadi sasa wamekuwa wakialikwa Walimu wa masomo mbalimbali na kufundisha masomo husika kulingana na Mtaala wa nchi yetu ya Tanzania.
Hatakama hakuna nafasi ya mwanafunzi kuuliza swali lakini naliona hilo ni hatua nzuri na ya kizalendo katika kukikuza kizazi chetu katika mwelekeo sahihi na kwa maana nyingine wazazi na wadau wa maendeleo ya Elimu pia wanapata fursa ya kutathimini Mtaala wa elimu yetu kwaujumla na baadae kuwa na uwanja wa kutoa maoni.
Sioni haja ya kuvitaja vyombo na asasi moja moja ili nisije nikawaacha wengine, lakini kwa pamoja Hongereni sana!