Pongezi kwa Tigo Tanzania

Nyakwec's Bro

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
820
174
Habari zenu Wakuu.

Napenda kutoa pongezi kwa Mtandao wa Tigo Tanzania kwa kutambua wateja wao muhimu na kuwapa kipaumbele kwenye huduma zao.

Juzi nilipiga simu Tigo huduma kwa Wateja(Namba 100) na kupokelewa na maneno yanayosema "Wewe ni mteja wetu wa Muhimu simu yako haitowekwa kwenye foleni" baada ya maelezo hayo simu yangu ikapokelewa na kuhudumiwa.

Kwakweli nimevutiwa sana na huduma hii ya haraka kwa wateja wa muhimu,sijui ni vigezo gani wametumia kutupata wao wanajua lakini kwa hivi karibuni kupiga simu katika hii mitandao yetu huduma kwa wateja imekuwa kero sana.Mitandao mingine hata namba za kuongea na Mhudumu haziko wazi lakini hata ukishaunganishwa unasubiri zaidi ya nusu saa ukiwa na tatizo la haraka inakuwa haina msaada.

Hongereni sana Tigo kwa huduma hii,endeleeni kuboresha huduma zenu Mitandao mingine waisome namba.

Ni hayo tu.
 
Hiy ni huduma ya kawaida , inaitwa tigo VIP waliselect wateja wachache kwa vigezo vyao (na walikua notified kupitia sms ) , wateja hao wakipiga simu huduma kwa wateja basi hujibiwa bila kusubiri.
 
Habari zenu Wakuu.

Napenda kutoa pongezi kwa Mtandao wa Tigo Tanzania kwa kutambua wateja wao muhimu na kuwapa kipaumbele kwenye huduma zao.

Juzi nilipiga simu Tigo huduma kwa Wateja(Namba 100) na kupokelewa na maneno yanayosema "Wewe ni mteja wetu wa Muhimu simu yako haitowekwa kwenye foleni" baada ya maelezo hayo simu yangu ikapokelewa na kuhudumiwa.

Kwakweli nimevutiwa sana na huduma hii ya haraka kwa wateja wa muhimu,sijui ni vigezo gani wametumia kutupata wao wanajua lakini kwa hivi karibuni kupiga simu katika hii mitandao yetu huduma kwa wateja imekuwa kero sana.Mitandao mingine hata namba za kuongea na Mhudumu haziko wazi lakini hata ukishaunganishwa unasubiri zaidi ya nusu saa ukiwa na tatizo la haraka inakuwa haina msaada.

Hongereni sana Tigo kwa huduma hii,endeleeni kuboresha huduma zenu Mitandao mingine waisome namba.

Ni hayo tu.
imethibitishwa umepokea........
 
Tigo ni limtandao la hovyo kabisa kuwah kutokea hapa tanzania,sijui hata wateja wa tigo huwa ni watu wenye akili gani!
 
Naungana na wewe 100% nilipoteza simu yangu yenye line ya voda nina line la Tigo nikasema nisipate shida kuhangaika kurenew ngoja niitumie tigo nilijuuuuuuuuuutaaaaa kabisa

nilijiunga na kifushi cha week 1 yaan siku 7 walianza kunitumia msg zilifika 300 kuniambia kwenye account yangu hakuna salio . Baada ya lile likifurushi kuisha niliitupa for good sitaki kusikai Tigo wala muamala wa Tigo
 
We unalako
 
Back
Top Bottom