Kenya 2022 Pongezi kwa Rais Samia kuwa 'Neutral' kwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya. Pole kwa Museveni na Kagame kwa 'Kumsapoti' anayeenda Kuangushwa

Kenya 2022 General Election

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,252
110,834
System ya Tanzania ilishausoma mapema Mchezo na kujua kuwa Ruto ataenda (na mpaka sasa GENTAMYCINE nasema ameshashinda) na Kumshauri Mama kutoonyesha Upande wake Wowote kati ya Ruto na Odinga.

Nazilaumu mno Systems za Uganda na Rwanda kwa Kukurupuka kwao na kudanganywa na Rafiki yao Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta kuwa Mtu anayemtaka Raila Odinga ndiyo atashinda na wao Marais Museveni na Kagame Kuingia 'Kichwakichwa' na waziwazi huku Wakijiamini wakisema wanamuunga mkono Raila Odinga.

Mpaka muda naandika huu Uzi ni kwamba asiyetakiwa na System ya Kenya na Adui Mkuu wa Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta Mgombea na aliyekuwa Makamu Rais William Ruto ameshashinda huu Uchaguzi.

Kinachofanywa sasa na System ya Kenya kwa Kushirikiana na Watu wa IEBC (Tume ya Uchaguzi Kenya ) ni Kumuibia Kura Mshindo William Ruto na kumpa Raila Odinga Ili atangazwe Mshindi.

Na endapo Mbinu hii itaonekana ni Hatari (Haifai) na Watu wa System ya Kenya kwa labda Kuhofia italeta Machafuko makubwa kinachoenda Kufanyika (Kufanywa) ni Kulazimisha 'Kubalansi' Matokeo ili kuwe na Marudio ya Uchaguzi na waweze Kumpiga (Kumuibia) vizuri Hustler William Ruto anayeonekana Kukubalika zaidi na Vijana hasa Wasio na Ajira na Wenye Maisha Magumu ya Kiuchumi.

Na karma kutakuwa na Marudio ya Uchaguzi huu basi bado Rais Uhuru Kenyatta atatakiwa kuwa Madarakani kwa Siku 90 (takriban Miezi Mitatu) na MImi GENTAMYCINE namshauri Hustler William Ruto kuwa kama anajipenda basi afanye kila awezalo ndani ya Siku hizi 90 asiwe Kenya na kama akiwa Kenya basi ajitahidi awe na Ulinzi mkubwa na mkali kwani najua nini Kitajaribiwa kufanywa Kwake ili kumdhoofisha au kumuua Nguvu kwani tayari System ya Kenya haimtaki kwakuwa imeshajua kuwa Ruto akiwa Rais wa Kenya ataanza Kulipiza Kisasi kwa Adui yake Mkuu Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta na pia atataifisha Mali zake nyingi na 'Kumpurula' kila Kitu Uhuru Kenyatta ambaye siyo Siri kuanzia Marehemu Baba yake na hata Yeye wameiibia mno Kenya ( hasa Ardhi ) na Wamejitajirisha sana kwa kuwa na Mali nyingi Ndani na Nje ya Kenya.

Pongezi nyingi tu Kwako Rais Samia.
 
Ahaa haaaah mtaani wangu bhana, unajua sana kucheza na akili za watu. Umejiweka ktk position ambayo utakuwa mshindi, yaani kama Agwambo, Baba akishinda basi kaiba kura. Usisahau huyo Hussler Ruto ni mafia vilevile, hashindwi kitu hata kuiba ana uwezo kwani naye ni 'Sonko', Mdosi ile mbaya. Pia swala la ukabila linambeba kwani anatoka kwenye Jamii ya Karenjin yenye watu wengi sana. Na huku Wakikuyu wakimpa support kwa vile running mate wake ni Mkikuyu. Vyovyote vile lolote linaweza tokea. Ila sisi wa kanda ya ziwa tungependa 'Omugaya' Raila ashinde kwani ana unasaba zaidi na ndugu zetu wa Rorya.
 
Mkuu hakuna anae kuchukia. Wewe ni kivutio ndio maana tunapenda kusoma.post zako.

Halafu wakurya hawakimbiliagi polisi mkuu. Kwa kukimbilia kwako polisi ume wa aibisha Wana mara wenzako.

Wewe hupendi challenge kumbe?

Anyways mada yako uliyo andika haina mashiko.

Unaweza kuweka uthibitisho kwamba Kagame na Museveni Wana msapoti Raila?

Hujui unafanya jambo la hatari sana kuwazushia viongozi wanao heshimika kama Kagame na Museveni?

U put jf into jeopardy kwa kuandika tuhuma za uzushi uzushi dhidi ya viongozi wanao heshimika

Acha utoto mkuu
 
Hakuna mshindi hadi sasa, tv za kenya kila moja ina takwimu zake, probably nyingi ni za mchongo
Kila kituo cha runinga kinajumlisha chenyewe na kuweka matokeo, wanavurugana sana.

Tulia tuone kinachoendelea
Acha mihemko yako
 
 
Mtani acha ufalla unajitetea kama wa kike ...acha mara moja wewe wakiume alaaa🤣
 
Odinga kuwa Rais maana yake nchi iko mikononi mwa Kenyata, Odinga hana akili za kuiongoza Kenya bali kinachofanyika ni kuwafurahisha wajaluo na kubalance mambo. Mwisho wa siku Odinga atakuwa ceremonial tu na gizani atakuwepo Kenyata.

Nakuunga mkono Genta, kama system itacalucate na kuona kumtangaza Odinga hali inaweza kuwa mbaya basi kitakachofanyika ni maridhiano na Odinga anaweza kuwa makamu huku Ruto akiwa mwenyekiti.
 
Dini imekukaa,jibu ni kuuchuna tu😘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…