Pongezi kwa kufuta pombe kali za viroba

Pongezi kwa kufuta pombe kali za viroba

mdesi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
1,375
Reaction score
2,267
Natumai wanajukwaa kuwa mu wazima,

Naomba niende moja kwa moja kwenye point yangu,

Ukichunguza na kulinganisha idadi ya ajali za vyombo vya moto hasa bodaboda, vijijini na mijini hakika vimepungua sana ukilinganisha na siku za nyuma. Nanyi wenzangu mtakuwa mashahidi.

Katika kuhoji na kuchunguza juu ya kupungua kwa ajali hizi, utagundua au kutambua kuwa ni baada tu ya serikali kupiga marufuku ya uuzwaji wa viroba ndipo idadi ya ajali za barabarani ukaanza kipungua. Madereva wanaendesha wakiwa na akili timamu na kwa tahadhari makini. Waendesha bodaboda sasa wanaheshimika kuliko hapo awali walichukuliwa kama wahuni. Idadi ya wakabaji na waporaji wa Simu umepingua kwa kiasi chake.

Napenda nimpongeze kwa dhati kabisa mtanzania aliye toa wazo ya kufuta viroba. Maana imeleta positive impact pamoja na kwamba sababu zilizotolewazilikuwa za kimazingira.

Naomba watanzania wengine tuwe na mawazo yenye tija kwa taifa na si mawazo ya kututia hasara.
 
Natumai wanajukwaa kuwa mu wazima. Naomba niende moja kwa moja kwenye point yangu, ukichunguza na kulinganisha idadi ya ajali za vyombo vya moto hasa bodaboda, vijijini na mijini hakika vimepungua sana ukilinganisha na siku za nyuma. Nanyi wenzangu mtakuwa mashahidi.

Katika kuhoji na kuchunguza juu ya kupungua kwa ajali hizi, utagundua au kutambua kuwa ni baada tu ya serikali kupiga marufuku ya uuzwaji wa viroba ndipo idadi ya ajali za barabarani ukaanza kipungua. Madereva wanaendesha wakiwa na akili timamu na kwa tahadhari makini. Waendesha bodaboda sasa wanaheshimika kuliko hapo awali walichukuliwa kama wahuni. Idadi ya wakabaji na waporaji wa Simu umepingua kwa kiasi chake.

Napenda nimpongeze kwa dhati kabisa mtanzania aliye toa wazo ya kufuta viroba. Maana imeleta positive impact pamoja na kwamba sababu zilizotolewazilikuwa za kimazingira.

Naomba watanzania wengine tuwe na mawazo yenye tija kwa taifa na si mawazo ya kututia hasara.
KWA UTAFITI UPI? ACHA POROJO, MBONA TOTI ZINAPIMWA VITUONI NA BODABODA WANAKUNYWA?
 
WaPo watakaokupinga sababu watanzania hawapendi vitu vizuri zaidi ya ulalamishi.
 
Janga la viroba litakumbukwa katika historia ya nchi hii,viroba vilikuwa vinawaua vijana kuliko vita vya Uganda.
 
Umenena mkuu alichosema mwenzetu kuhusu viroba ni kweli kabisa toka vipigwe marufuku ajali zimepungua hata nidhamu kwa vijana ipo, Mungu angeweka neema tukaweza kufanikiwa madawa ya kulevya na bangi tukaokoa jamii kwa ujumla aliyekujibu vile huenda ana bodaboda
 
KWA UTAFITI UPI? ACHA POROJO, MBONA TOTI ZINAPIMWA VITUONI NA BODABODA WANAKUNYWA?
Kwa muono wako unadhani nini kimechangia kupungua kwa hizi ajali?
 
Vijana walikuwa wamefanywa kama "zombies" na baadhi ya wanasiasa,walikuwa wananyweshwa viroba halafu wanapakiwa kwenye mafuso bila kujitambua wanapelekwa kwenye mikutano huku wakishangilia tu bila kujua wanashangilia nini.
 
Back
Top Bottom