mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,419
- 17,759
Nimetafakari nikaona hawa jamaa tusiwabeze. Wanawakilisha Jamii ya watanzania wavumilivu.
1: Wanaingia katika uchaguzi wakiwa katika kumbukumbu ya suluba Kubwa ya wasioulikana ambao hawajajulikana. Kati ya CCM, Wananchi, na Wapinzani tukiacha wale Ndugu wa kibiti wapinzani wameongoza kwa kusurubiwa na wasiojulikana. Hivyo hii imehafifisha juhudi zao na kuwapa competitive disadvantage.
2: Mtaji wa mpinzani ni mdomo na mapungufu ya anayetawala. kuzuiwa kufanya mikutano na wananchi, kukamatwakamatwa wakiwa mikutanoni mwao kunawapa competitive disadvantage dhidi ya CCM ambao kupitia Serikali waliyokuwa wanaongoza wamejinadi miaka 5 wakati wenzao wana miezi tu.
3: Kuhama kwa Watu wao wakubwa tena kwa kushtukiza kumeidhohofisha safu yao pakubwa.
4: Upungufu wa fedha unaodaiwa kuwakumba ulipaswa kuwafanya washindwe hata kunadi madiwani lkn nawaona bado wanakomaa tu.
5: Janga LA Corona lilipaswa kufunga kabisa Ofisini zoteza Wapinzani. Walikuwa wako upande wa Ugonjwa wakati Rais alikuwa upande wa uwezo wa Mungu kuliteketeza Janga.Rais ameshinda wao wameshindwa. Kumbuka zaidi ya 95% ya watanzania watakaopiga kura naamini wanamuamini Mungu na miungu kwa jinsi zao. Hili tu lilitosha kukausha mafuriko ktk mikutano yao lkn angalau watu wanajaa.
6:Binge Giza. Siku zote wapinzani wamkuwa wakija kwetu wananchi wakiwa wameshajitambulisha kutokea Bungeni. Wameshaonyesha uwezo wao Mkubwa dhidi ya mamia ya wabunge wa CCM. Ni kupitia Bunge tulijua nani anaweza hata akawa rais, nni na so nani kwenye uchungu na nchi. Kuliondoa Bunge live ni kuwanyima competitive advantage wapinzani. Kuweka live kila tukio LA Rais na Serikali, Kuweka live Bunge pale tu serikali inapoelezea mazuri yake ni kuwanyima kabisa pumzi wapinzani.
7: Kurudi kwa CCM Lowassa na Sumaye. Hawa jamaa kurudi CCM kulionyesha kabisa wapinzani walipodhani wamebakiza shoka moja tu kuangusha CCM sasa KAZI imeanza upya. Matukio hata yalileta uchovu Mkubwa wa kihisia kwa Wapinzani. Ukiwaona wanakomaa Leo wapongeze.
Nimekuwa nikipita nikiangalia Ofisini mbalimbali za chadema miaka hii mitano nyingi zilikuwa haziko operational. Nyingi makufuli yana kutu, nyasi kila Kona.
Tuwe wakweli, tuwe wawazi Tukiwaona wapinzani wanapambana Leo lazima tuwashangae na sio kuwabeza maana hawakutakiwa kuwepo kwa Sifa saba hapo juu.