Pongezi: Appreciation tweet for Hashim Spunda Rungwe

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Anaandika ZAKAYO MBAGA. (Huko twitter)

Miaka michache iliyopita nilikuwa na uhitaji wa msaada wa kimahakama (Kuthibitisha vyeti kwa Wakili) ikiwa ni mchakato wa kawaida katika utafutaji wa ajira.

Nilienda law firm moja maeneo ya makumbusho lakini bei niliyotajiwa kwa cheti kimoja sikuwa na uwezo wa kuilipa kwa wakati huo hata kama ningeambiwa ni kwa ajili ya vyeti vyote achilia mbali cheti kimoja tu.

Wakati narudi ghetto K/nyama kupitia Bahari motors ambapo ndizo ofisi za mzee wetu huyu nikajishauri niingie kumuona kwa ajili hiyo.

Ila nikajisemea, pale nilipotoka gharama ni kubwa vile sembuse hapa kwa wakili wa mahakama kuu?
Nikapiga moyo konde nikaingia kumuona. Alinikaribisha vizuri sana na nikamuelezea shida yangu lakini hasa nikiwa interested na issue ya bei ili kama siiwezi nisimpotezee muda.

Akaniambia wewe toa kwanza vyeti tuvione, tunapangaje bei ilihali kazi haijafanyika?😁😁
Kiukweli hii kauli ilinitisha sana😂, nikatoa lile lundo la vyeti pale nikamuwekea mezani. Moja kwa moja akatoa mhuri akaanza kupiga na kuvisign huku akinipigisha story za hapa na pale.

Mwisho niliulizia bei ya huduma akaniambia wewe ndio kwanza unatafuta kazi, huwezi kumlipa Wakili,😁 toa tu kile unachoweza kwa sasa uende ukapambane. Kiukweli sikuamini nilichokisikia😂😂. Nikatoa shuka moja la kimasai nikamshukuru mzee wangu tukaagana nikaondoka.

I appreciate

(IMENIVUTIA)
 
Anataka kugombea tena mwaka huu?
 
A.k.a Sauti ya Zege. Huyu amepooza siasa zake za kizee zingenoga Kama (Marehemu)Mch Mtikikila angekuwepo.
 
Attachments

  • images (25).jpeg
    images (25).jpeg
    25.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom