tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameeleza wasiwasi wake kuhusu wafanyabiashara wenye ushawishi mkubwa serikalini akisema hali hiyo ni tishio kwa maslahi ya wananchi wa kawaida.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mtangazaji Wilberforce Ngoto kupitia kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV, Sheikh Ponda ambaye pia ni mwanachama wa ACT-Wazalendo, amejibu swali kuhusu mtazamo wake kuhusiana na wafanyabiashara wakubwa kuchangia harambee ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Soma pia: Shehe Issa Ponda kushinda jimbo la Temeke mchana kweupe - Mikiki katika kutetea wanyonge ndio turufu yake Temeke
Sheikh Ponda amesema kuwa ni hatari kwa taifa pale wafanyabiashara wanapopewa nafasi au ushawishi mkubwa katika maamuzi ya serikali kwa sababu wanapendelea maslahi yao binafsi kuliko maslahi ya wananchi wa hali ya chini.
“Wafanyabiashara katika mataifa yote ukiwaacha wakawa na ushawishi katika serikali wanatengeneza tatizo kubwa kwasababu wao ni watu wa maslahi na maisha, wanajali maisha yao, huwa hawamjali mtu wa maisha ya chini”, amesema Sheikh Ponda.