Aloyce Mkwizu
Member
- Dec 19, 2016
- 70
- 53
NA: ALOYCE MKWIZU.
Pombe sio chai wala maji ya kunywa. Pombe sio mboga kwamba lazima ule na chakula. Pombe sio dawa useme nipo kwenye dozi ya mwaka. Vijana wanawaiga wazee kunywa, wamesahau methali inayosema kuwa "ukimuiga tembo kunywa, utachanika msamba." Pombe sio mbaya ila madhara yake ndio mabaya. Kwanini ujitese wakati kuna juisi na maziwa.
Walevi wangapi wanataka;
- Kisukari.
- Matatizo ya moyo.
- Saratani ya ini.
- Msongo wa mawazo.
- Kusinyaa kwa ubongo.
- Ugonjwa wa kongosho.
- Kupoteza hisia.
- Shinikizo la damu.
- Anemia.
- Maumivu ya misuli.
- Kusinyaa kwa uso.
- Kuharibika kwa mfumo wa uzazi.
- Kitambi na kunenepa ovyo.
Wahenga walisema "Sikio la kufa halisikii dawa."
Kwa ushauri nasaha:
+918448628500
aloycemkwizu99@gmail.com