Pombe si Chai, Aibu! Aibu! Aibu!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KATIKA kuonyesha kuwa mmomonyoko wa maadili unashika kasi kila kukicha nchini Tanzania, wapenzi wawili jana wameonekana wakifanya mapenzi hadharani kwa kuzidiwa na pombe kupita kiasi huko maeneo ya Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.
Wapenzi hao ambao walizidiwa na pombe walijikuta wakifanya mapenzi hadharani kwenye majani yaliyokuwa yameota katika moja ya njia ya maeneo hayo.

Tukio hilo lililoshangaza wapita njia waliowengi lilikuwa likifanyika majira ya saa 3 usiku eneo hilo.

Tukio hilo lilikuwa ni la aibu na la kusikitisha kwa kuonekana wapenzi hao wakiwa wamelala michangani wakiendelea na vitendo vya kimapenzi hadharani bila hata chembe ya aibu.

Kutokana na tukio hilo ambalo lilizua tafrani maeneo hayo hasa kwa wale wastaarabu baadhi ya wapita njia walionekana na mtandao huu waliokuwa wakihitaji kupita njia hiyo wakiwa na watoto wao walilazimika kukimbia huku wengine wakilazimika kubadilisha njia ili kunusuru watoto waisone tukio hilo.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wanaoishi maeneo hayo, waliokuwa na moyo kuwasogelea wapenzi hao walidai kuwa, wawili hao walikuwa wakionekana maeneo hayo mara kwa mara wakiwa wanaongozana kwenda kwenye vilabu zinavyouza pombe za kienyeji kwenda kupata vinywaji hivyo na walikuwa hawafahamiki walikuwa wanaishi eneo lipi.

Hata hivyo mwandishi wa habari hii hakufanikiwa kupata majina ya wawili hao, na imeona kutoweka picha kwa kuwa picha hiyo kimaadili isingeweza kutumika katika mtandao huu kutokana na kuwa kinyume na maadili ya watanzania.
 
hayo ni mataputapu ....!


hivi ndivyo vitu
beerobama-300x246.jpg
 
tatizo la kilaji kikiishapanda kichwani hukawii kwenda kupimwa akili nakumbuka yamewahitokea hayo last year!ila akaonekana yupo ok
mkulu anakunywa banana .... ukipiga mbili tu akili zinakaa tenge....ha haaaaaa
 
tatizo la kilaji kikiishapanda kichwani hukawii kwenda kupimwa akili nakumbuka yamewahitokea hayo last year!ila akaonekana yupo ok

mhusika ni nani mkuu ..... pia wapo wakulu wengi tuu wanatumia ule moshi mmene ....hukawii kukurupuka ukishatumia..... ha haaaaaaaaaa
 
ndio maana nchi imechanganyikiwa kabisa wamekosa maadili inawezekana hata machozi ya simba wanagonga sijui tutaishia wapi
mhusika ni nani mkuu ..... pia wapo wakulu wengi tuu wanatumia ule moshi mmene ....hukawii kukurupuka ukishatumia..... ha haaaaaaaaaa
 
kama sijakosea hii ni mbege toka kaskazini mwa tanzania kwa wachaga kilimanjaro!hii kitu nimegonga sana kipindi nipo o level tulikua tunatoroka shule kwenda kwa mama mmoja hv pale ir

umepatia

hii kitu sio mchezo ...ukigonga hii lazima uburudike
 
huwezi kukuta mtu anaetumia mjani AKA kijiti anafanya mambo a aibu namna hii.....
 
Back
Top Bottom