Pombe na sigara vyaleta mtafaruku katika ndoa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pombe na sigara vyaleta mtafaruku katika ndoa...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kashaijabutege, Dec 21, 2010.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kuna rafiki yangu kaniambia kuwa mkewe amemuomba watengane vitanda kwa kuwa mama hataki harufu ya pombe na sigara. Rafiki yangu hataki kufanya hivyo kwa kudai ndoa ni kuvumiliana; na zaidi kuwa walipooana miaka 10 iliyopita pombe na sigara halikuwa tatizo; isipokuwa kuanzia mwaka jana ambapo mkewe alimpokea Bwana Yesu na kuyaacha ya kale. Rafiki yangu anasema yuko tayari kuoa mwanamke mwingine badala ya kuacha mazoea yake au kulala vitanda viwili wakiwa wanandoa.

  Mnawashaurije wanandoa hawa?
   
 2. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  basi mshauri aache sigara....pombe inavumilika kidogo....khaaaa
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Inabidi na huyu mwanaume ampokee bwana ni kweli harufu ya pombe na sigara ni kero kama wewe si mtumiaji
   
 5. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Je akiacha sigara na pombe bila kumpokea Bwana haitasaidia?
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sikuelewi, mabwana wawili ni wapi? Na ni nani anawatumikia?
   
 7. E

  Exav Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Napata mashaka sana na uamzi wa kutengana vitanda! Kama mama amempokea Bwana Yesu, abebe mzigo wa maombi ili mume wake naye abadilike. Fikiria hivi:

  Kabla mama hajampokea Bwana Yesu ==>> ndoa haina matatizo
  Mama kampokea Bwana Yesu ==>> anataka watengane vitanda na mumewe eti kwa kuwa mumewe bado ni mtu wa sigara+pombe

  Huyu mwanamume ambaye hajampokea Yesu, si atakuwa na mashaka ya kumpokea Yesu kwa kuzingatia hayo matokeo?? Anajifunza nini juu ya Yesu? Hii si ni sawa na kulifanya jina la Yesu litukanwe?

  Huyo mama kama kweli kampokea Bwana Yesu na akayaacha ya kale; anyenyekee, aongeze upendo kwa mume wake, amwombee kwa dhati sana mume wake. Ageuke kabisa 180 degrees kumwelekea Yesu, na awe anamshirikisha mume wake hatua kwa hatua katika kujifunza neno la Mungu. Naamini kabisa kumpokea Bwana Yesu siyo sababu ya kutengana vitanda - hii ni kinyume na haipendezi kabisa. Mungu anakuchukia kuachana.
   
 8. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Baba ampokee bwana na Mama anye pombe na sigara
   
Loading...