Faru John II
Senior Member
- Dec 27, 2016
- 134
- 135
(POMBE: ni kweli mna nguvu lakini sio kwa kiwango hicho)
PEPO YA MABWEGE
Kumekuwepo na vitisho dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari ktk taifa letu, jambo la kusikitisha zaidi vitisho hivi vinatoka mamlaka ya juu kabisa ya Utawala. Vitisho hivi vinalenga kutoa muongozo kwa vyombo vya habari yakiwemo magazeti kuacha kuweka vichwa vya habari vyenye lengo la kuikosoa serikali pale inapokiuka sheria za nchi kwa kutumia mamlaka yake visivyo.
Jambo la ajabu zaidi ni pale ambapo vyombo binafsi vya television vinapotishwa kuacha habari zinazoripoti kuhusu vilio na maandamano ya wakulima ambapo imewahi kuripotiwa kukamatwa kwa Mwandishi Khalfani Liundi kutokana na kuripoti juu ya maandamano ya wakulima.
Vitisho hivi vimeendelea mpaka kwa baadhi ya Wabunge kutoka kwa viongozi wa serikali kuwatenza nguvu ya kuripoti dhulma na uonevu unaofanywa dhidi ya Raia wasiokuwa na hatia.
Matumizi haya ya nguvu kupita ukomo wa katiba ya Nchi yakiendelea yatahatarisha amani na ustawi wa taifa letu. Hapa ni Tanzania sio Somalia, tunahitaji kukemea vitisho dhidi ya uhuru wa habari na vyombo vya habari.
Lisilo kubalika kufanyiwa mwanachama wa CCM lisikubalike pia kufanyiwa mwanachama wa chama chochote na hata asiyekuwa na chama.
Asiwadanganye mtu, migogoro mingi inayotokea duniani na iliyowahi kutokea na kuvuruga amani ya nchi chimbuko lake ni watawala walioamua kulinda maslahi binafsi au maslahi ya wachache, kuruhusu Uonevu, dhulma na Ufisadi, usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi nk.
Wito wangu kwa viongozi na watumishi wa umma, watambue kuwa nguvu waliyonayo ina ukomo kikatiba na nguvu hiyo haitumiki kinyume na muongozo unaopatikana katika katiba yetu.
Ni kweli serikali inafanya juhudi kubwa ya kuwaletea Wananchi wake maendeleo, lakini maendeleo haya hayatokuwa na tija ikiwa watu watajengewa nidhamu ya woga, watendaji watakapo ogopa kuchukua hatua wakiogopa kutumbuliwa bila hatia, vyombo vya habari vitakapo wacha jukumu la kumulika madudu ya serikali kwa kuogopa vitisho vikirejea tukio la mwangosi.
VYETI KWANZA, VITISHO BAADAE